The House of Favourite Newspapers

Tarimba: “Tunalipa Hadi Bilioni 2 Kwa Mwezi, Sportpesa” – Video

0

ABBAS TARIMBA, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa SportPesa Tanzania, amesema mafanikio makubwa ya kampuni hiyo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ushirikiano wanaoupata kutoka kwa wadau wake wa karibu ikiwa ni pamoja na Kampuni ya Global Publishers.

Ameyasema hayo  alipotembelea Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori Dar es Salaam ambapo ziara hiyo imekuja katika kutimiza miaka mitatu kwa Kampuni ya SportPesa Tanzania.

 

“Tumekuwa tukifanya kazi kwa ukaribu na watu mbalimbali, na tulianza taratibu kwani kulikuwa kuna kampuni nyingine ambazo zinafanya kazi, ila kwa ushirikiano mkubwa ambao tumekuwa tukiupata kutoka kwa wadau na Kampuni ya Global hasa kwa upande wa magazeti ya michezo ambayo ni Championi na SpotiXtra, tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

 

“Mbali na kufanya kazi kwa mafanikio makubwa pia tumekuwa tukilipa kodi kwa Serikali zaidi ya bilioni, hivyo sio kitu kidogo hasa ukizingatia kwamba maendeleo ya Serikali yanahitaji kodi nasi pia tumekuwa tukilipa kodi.

 

“Wadau ambao wapo pamoja nasi tunaomba ushirikiano wao kwani bado tunazidi kupambana ili kuwa bora na mambo yote tunayafanya kwa weledi na kuzingatia kanuni ambazo zipo,” amesema Tarimba.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply