The House of Favourite Newspapers

TAXIFY YAZINDUA HUDUMA MPYA YA ‘TAXIFY BOMBA’ JIJINI DAR

Taxify, inayokuwa kwa kasi Ulaya na Afrika katika huduma ya usafirishaji leo Julai, 12 2018 jijini Dar imetambulisha huduma mpya ya ‘TaxifyBomba’ maalum kwa magari madogo, Dar es Salaam, Tanzania.

 

Kampuni hiyo inajaribu kupanua chaguzi za wasafiri na kuruhusu madereva wa magari madogo ambayo yanatumia matumizi madogo kujipatia fursa ya kipato.

 

TaxifyBomba ni daraja rafiki kwa jamii kutokana na nauli ndogo na faida kubwa kwa madereva. Daraja hili linahusisha magari madogo yenye viti vinne hususani yenye 1300cc na injini inayofaa kwa huduma za kila siku.

 

Haya ni magari yenye injini ndogo ambazo hutumia mafuta kidogo, na kusababisha gharama za chini za uendeshaji kwa madereva na hivyo kuwezesha utoaji huduma za bei nafuu kwa wasafiri.

 

Remmy Eseka, Meneja Uendeshaji nchini Tanzania alieleza kuwa, “Tumebaini kuwa, msingi wa wateja wetu umepanuka. Kwa sasa watu wamefikia mahali ambapo wanataka chaguzi nyingi zaidi za usafiri na jinsi wanavyoweza kufanya safari zao ndani ya jiji. Pia kuna ongezeko kubwa la madereva ambao wanataka kutumia magari yenye injini ndogo. Huduma hii inakidhi mahitaji ya madereva na watumiaji.

 

TaxifyBomba imetoa punguzo la asilimia 30 ya fedha ambapo nauli itaanzia sh. 800, sh. 210 kwa kilomita moja, sh. 50 kwa dakika na usafiri wa chini sh.2,000.

 

“Bei za daraja hili zimeundwa kwa uangalifu wa hali ya juu ili kuwapa nafasi wasafiri  kwenda popote ikiwa ni fursa moja wapo pia ya kuwawezesha madereva kupata zaidi. Madereva watakuwa na nafasi ya kufanya safari nyingi kupitia daraja hili jipya,” alielezea Remmy.

 

Taxify imeongeza uvumbuzi zaidi na kuelewa mahitaji ya madereva na wasafiri wanaotumia huduma hiyo.

 

Taxify Bomba inatambulishwa ikiwa ni miezi michache tu baada ya uzinduzi wa TaxifyBajaji (chaguo la usafiri wa Bajaji) na Taxify XL (magari yenye viti sita).

Comments are closed.