The House of Favourite Newspapers

TECNO Kuwapa Furaha ya Krismasi na Mwaka Mpya Wateja Wake

0
Meneja Uhusiano wa Tecno hapa nchini, Eric Mkomoye (kushoto) alipokuwa akitangaza neema hiyo kwa wateja wa TECNO.

Kampuni ya simu za mkononi ya  TECNO inaendelea kuwakumbusha wateja wake kutembelea maduka ya TECNO katika msimu huu wa Krisimasi na mwaka mpya.

Akizungumza na wanahabari Meneja Uhusiano wa TECNO hapa nchini, Eric Mkomoye amesema kampuni hiyo  ilizindua rasmi promosheni ya TUNARUDISHA FURAHA NYUMBANI terehe 11/12/2020 ambapo mteja atakayenunua TECNO Camon 16s na Spark 5pro basi moja kwa moja atakuwa ameingia kwenye droo ya kushindania Mashine ya kufulia, Flat TV, Blenda, Rice cooker na zawadi nyenginezo hutolewa papohapo.

Wateja wakichangamkia promosheni hiyo.                    

TECNO itakuwa ikitangaza washindi wa Promosheni hii ya TUNARUDISHA FURAHA NYUMBANI kwa awamu mbili, droo kubwa ya kwanza itafanyika tarehe 19/12/2020 ambapo zawadi zitakazotolewa ni Mashine ya kufulia, Gift vocha na kifurushi  chenye zawadi mchanganyiko za Krisimasi na droo ya pili kuchezeshwa 7/1/2021 kupitia Instagram account ya @tecnomobiletanzania.

Watoa huduma wa TECNO wakiwa kwenye promosheni hiyo.

Kwa kujikumbusha kwa ufupi TECNO Spark 5pro na TECNO Camon 16s ni matoleo mapya kwa kampuni ya TECNO lakini pia ni simu pendwa kutokana na uwezo wake katika upande wa camera na kimuonekano kwa ujumla.

Camon 16s;

Ni simu yenye kamera kali kuzidi simu zote za TECNO nyuma ikiwa na MP 48 na selfie ni MP 16, ukubwa wa memory ni 128GB+4GB RAM na betri lenye kudumu na chaji kwa muda mrefu la mAh 5000.

Spark 5pro;

Ni simu inayolenga watu wenye uchumi wa hali zote, ina camera yenye uwezo wa kuchukua picha wakati wowote haijalishi ni wakati gani na katika mazingira gani, camera ya Spark 5pro ni MP16 na selfie yenye MP 8, memory ya GB 64+GB 3 RAM huku ikiwa na betri lenye mAh 5000.

Kwa maelezo zaidi tembelea https://www.tecno- obile.com/tz/home/

Leave A Reply