The House of Favourite Newspapers

TETEMEKO LA ARDHI LAUA MMOJA SONGWE

MKAZI mmoja wa Kijiji cha Iyula, Kata ya Iyula wilaya ya Mbozi, SONGWE, Mwanji Mtega amefariki dunia kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea jana Alhamisi, Machi 21, 2019, mchana katika maeneo mbalimbali ya mkoani humo.

 

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, GEOGRE KYANDO amesema Mwanji alifariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta ya nyumba aliyokuwa anaishi.

 

Tetemeko hilo lililodumu kwa takriban dakika mbili na katika mikoa ya Mbeya na kuzua taharuki huku baadhi ya wananchi na wafanyakazi katika ofisi mbalimbali wakitimua mbio. Baadhi walilazimika kuacha ofisi zao huku waliopo majumbani wakitoka nje ya nyumba zao.

Comments are closed.