The House of Favourite Newspapers

TFF Mkicheza Makida Kwa Timu ya Vijana, Mtalitia Aibu AFCON 2019

0
Rais wa Tff Wallace Kiria.

TANZANIA itakuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 mwaka 2019, ambapo mataifa kadhaa yatawasili hapa nchini kwa ajili ya kinyang’anyiro hicho kikubwa na chenye heshima ya aina yake barani hapa.

 

Sote tunafahamu kwamba hii ni nafasi ya pekee kwa taifa letu kupata heshima kubwa ya aina hiyo ambayo haijawahi kutokea katika historia ya nchi yetu na kwa vyovyote vile taifa linalokuwa mwenyeji mara nyingi hufanya maandalizi mazito ili kuwepo na uwezekano wa kulibakisha kombe nyumbani.

 

Naunga mkono uongozi uliopita wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya Rais Jamal Malinzi, ambaye aliweka mipango ya kuwaandaa vijana wadogo chini ya umri wa miaka 15 ili mpaka kufikia mwaka 2019 wawe tayari kuunda kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys) kama timu yetu tegemeo katika patashika hizo za Afrika.

 

Katika mipango hiyo ya maandalizi nakumbuka Malinzi alifunga safari kutoka Dar es Salaam mpaka mkoani Mwanza ikiwa ni ziara ya siku moja kutembelea kituo cha mpira wa miguu kwa vijana cha Alliance kwa lengo la kuangalia jinsi kituo hicho kinavyoende sha shughuli zake ili TFF iweze kushirikiana nao kwa karibu.

 

Ziara hiyo ya Malinzi, akiambatana na Ayoub Nyenzi ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana pamoja na Ramadhan Nassib ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, kwangu niliona ni ya mafanikio makubwa kwa kuwa pande zote mbili zilikubaliana vijana wetu wakalelewe kwenye kituo hicho mpaka wakati watakapohitajika kulitumikia taifa katika michuano tunayoisubiri kwa hamu kubwa.

Lakini licha ya mipango hiyo kuwekwa sawa na vijana 22 kupelekwa kwenye kituo hicho huko jijini Mwanza, nilishituka kusikia malalamiko kutoka kwa mkurugenzi wa kituo hicho, James Bwire, kwamba TFF imevunja makubaliano waliyoafikiana kwamba itawahudumia vijana hao kwa mahitaji yote ya msingi ikiwemo pia kupeleka vifaa vya michezo kwenye kituo hicho.

VIDEO:Amber Lulu Anaswa Laivuuu Na Msanii Wa Burundi, Gaga

Hivi ninyi TFF mmewaza kitu gani mpaka mkafikia hatua ya kuwahudumia vijana 12 tu kati ya 22 ambao mmewapeleka kwenye kituo? Mlitaka nani awahudumie hao wengine waliobaki? Na kama mlijua hamna uwezo wa kuwa wenyeji wa kuhodhi michuano mikubwa kama hiyo kitu gani kiliwasukuma kuitamani nafasi hiyo adhimu?
Sitaki kujua ni nani wa kumbebesha lawama kwenye hili la kuwatelekeza watoto wetu kule Mwanza, isipokuwa makala haya nayaelekeza kwa TFF nzima kama taasisi yenye dhamana ya kusimamia maendeleo ya mpira wa miguu katika nchi yetu.

 

Upo msemo usemao mtu huvuna alichokipanda na hapa msije kushangaa Tanzania licha ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo, lakini wakati patashika zinaendelea ikawa msindikizaji namba moja na kuyaacha mataifa mengine yakitamba katika ardhi yetu na kujikuta taifa linapata aibu eti kwa sababu ya kuwepo kwa maandalizi duni ya wachezaji wetu.

 

Juzi Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao uliambatana na mkurugenzi wa michezo kutoka wizarani, Omary Singo, kwenda Mwanza kukutana na uongozi wa Kituo cha Alliance kuona ni jinsi gani mtafufua tena makubaliano ya kuwatunza vijana wetu mliowatelekeza kule, ni hatua nzuri lakini hakikisheni mnatimiza majukumu yenu kwa vitendo na siyo porojo.

 

Hili ni fundisho kwenye uongozi mpya mlioingia madarakani kwa kile mlichokiita kutaka kuokoa soka la Tanzania lisitokomee gizani, hakikisheni mnawekeza nguvu katika malezi ya vijana wetu ili wawe msaada mkubwa katika mapambano ya kulibakiza kombe hapa nyumbani.

Kutana na Patrick Rweyemamu, Meneja wa Simba Aliyemuibua Jonas Mkude

Leave A Reply