TFF Yalaani Mwandishi wa Habari Kupigwa na Polisi

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini(TFF), limelaani vikali kushambuliwa kwa Mwandishi wa Habari za Michezo, Sillas Mbise.

 

Kupitia Afisa Habari wake, Cliford Ndimbo, taarifa ilisema TFF imepanga kukutana na uongozi wa chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini TASWA kwaajili ya kujadiliana kuhusu tukio hilo na hatua stahiki za kuchukua.

 

Mwanahabari huyo, alishambuliwa na Askari wa Jeshi la Polisi siku ya tarehe 8 Agosti mwaka huu wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya Simba na Asante Kotoko ya Ghana.

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment