The House of Favourite Newspapers

Thamani ya Mbwana Samatta Yapandishwa Ulaya

 

Wilbert Molandi | CHAMPIONI |Dar es Salaam

NEEMA imezidi kumuangukia mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayekipiga Klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji, baada ya thamani yake kuongezeka kwa mara nyingine.

Samatta aliyewahi kuichezea Simba kabla ya kutimkia TP Mazembe, thamani yake ilianza kupanda Machi 22, mwaka huu na kufikia euro milioni 2.2 (zaidi ya Sh bilioni 5).

Mtanzania huyo, alijiunga na Genk Januari 29, mwaka jana kwa ajili ya kuichezea timu hiyo inayoshiriki Ligi ya Ubelgiji.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Transfermarket thamani ya mshambuliaji huyo ilipanda juzi Jumatatu na kufikia euro milioni 3 (sawa na shilingi bilioni 7.1)

Ni historia kubwa kwa mshambuliaji huyo Mtanzania kuingia kwenye ushindani wa wacheza soka duniani ambao thamani yao inaongezeka kwenye mauzo.

Samatta, thamani yake imeongezeka baada ya kuifungia mabao sita timu yake ya Genk kwenye michezo saba aliyocheza hivi karibuni ukiwemo mmoja ule wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wakati Taifa Stars iliposhinda mabao 2-0 huku mabao yote yakifungwa na mshambuliaji huyo wa Genk.

Mabadiliko hayo ya thamani yamefanyika Machi 30, mwaka huu katika wiki aliyofanya vizuri kwa kufunga mabao matatu.

Alifunga mabao mawili dhidi ya Botswana siku ya Jumamosi ya Machi 25 kabla ya kuwahi Ubelgiji na kufunga bao wikiendi iliyopita katika ushindi wa mabao 4-0 walioupata.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe nisiasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.