The House of Favourite Newspapers

The Angels of The Darkness-(malaika wa giza)-71

1

Watoto wawili mapacha, Arianna na Brianna wanatenganishwa wakiwa bado wadogo kufuatia tukio baya la kigaidi linalotokea wakiwa mapumzikoni na wazazi wao nchini Kenya, kwenye kituo kikubwa cha biashara cha Kikuyu Mall jijini Nairobi.

Katika tukio hilo, baba wa watoto hao, Joseph Ndaki, Meneja wa Benki Kuu ya Tanzania, Tawi la Dar es Salaam na mkewe, Asia Mustafa wanapigwa risasi na magaidi hao na kupoteza maisha, wakiwaacha watoto wao wakiwa bado wachanga.

Kila mmoja anapitia maisha tofauti kabisa, Arianna anarejeshwa Tanzania wakati Brianna anaokotwa na mwanamke mwendawazimu, Mashango ambaye anaishi naye kwenye mtaa wa watu maskini jijini Nairobi uitwao Mathare.

Arianna anapata bahati ya kukutana na Msuya, mfanyabiashara mkubwa ambaye anampenda kwa dhati na kuamua kumuoa. Baadaye, Arianna ananasa ujauzito wa Diego na wanapanga njama za kutoroka.

Msichana huyo anafanikiwa kutorokea nchini Kenya, jambo linalomfanya Msuya atangaze dau nono kwa atakayefanikisha kupatikana kwake. Hatimaye, pacha wa Arianna, Brianna aliyekulia kwenye mitaa ya watu maskini Mathare, Nairobi nchini  Kenya anapatikana na kuchukua nafasi ya Arianna  lakini anaonesha tofauti kubwa ya kitabia, jambo linalomshangaza kila mtu.

Upande wa pili, Arianna amewasili kwenye Mji wa Mandera lakini anajiovadozi madawa ya kulevya na kusababisha anusurike kupoteza maisha.

Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…Harakaharaka Arianna aliunganishwa na mashine ya kumsaidia kupumua kisha akatundikiwa dripu za dawa na maji zilizoanza kutiririka kwa kasi kuingia kwenye mishipa yake ya damu.

“Why such a beautiful young lady like her is endangering her life by using drugs?” (Kwa nini msichana mdogo na mrembo kama huyu anahatarisha maisha yake kwa kutumia madawa ya kulevya?) madaktari walikuwa wakiulizana wakati wakiendelea kumhangaikia Arianna huku kukiwa hakuna dalili zozote za msichana huyo kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Wakati matibabu yakiendelea, Dokta Faheem Omondi aliyekuwa akiongoza matibabu ya msichana huyo, aligundua jambo jingine lililomshtua sana.

“You need to see this!” alisema Dokta Faheem akiwaambia wenzake kuna jambo walitakiwa kuliona kuhusu mgonjwa waliyekuwa wakiendelea kumhangaikia, wote wakaacha kila walichokuwa wanakifanya na kumsogelea daktari huyo, akamfunua Arianna upande wa kuanzia kiunoni kushuka chini.

“Ooh! My God! Was she pregnant?” (Ooh! Mungu wangu, alikuwa mjamzito?) alisema daktari mwingine baada ya wote kushuhudia Arianna akitokwa na damu nyingi sehemu zake za siri, dalili kubwa ya mtu ambaye ujauzito wake umeharibika.

Tukio hilo liliwasikitisha sana madaktari na manesi wote waliokuwa ndani ya chumba hicho cha wagonjwa mahututi. Hawakuelewa iweje msichana huyo mrembo ajiingize kwenye matumizi ya dawa za kulevya wakati akijua fika kwamba alikuwa mjamzito.

Ilibidi kazi nyingine ya kujaribu kuokoa kiumbe kilichokuwa tumboni ianze lakini tayari walikuwa wamechelewa kwani ukichanganya madawa ya kulevya aliyokuwa ametumia na dawa alizopewa hospitalini hapo kwa ajili ya kuokoa maisha yake, zilitosha kukimaliza kabisa kiumbe kilichokuwa tumboni.

Baada ya kuridhika kwamba hakukuwa na namna ambayo wangeweza kusaidia kuokoa kiumbe kilichokuwa tumboni, walichokubaliana ni kusubiri msichana huyo arejewe na fahamu zake kisha taratibu za kumsafisha kizazi zianze. Kazi iliendelea lakini kila mmoja alionesha kuguswa sana na kilichotokea.
“Ndugu zake wako wapi?”
“Ameletwa na meneja wa hoteli, anasema ni mteja wake lakini hakuna anayefahamu taarifa zake zaidi, labda mwenyewe akizinduka ataeleza ametokea wapi kwani kwa kumtazama, haoneshi kama ni mkazi wa Mandera,” madaktari waliendelea kujadiliana huku matibabu ya msichana huyo yakiendelea.

Baada ya saa nyingi kupita, majira ya saa tano za usiku, nesi aliyekuwa amesalia ndani ya chumba alicholazwa Arianna, alishtuka baada ya kumuona msichana huyo akifumbua macho na kuanza kuangaza huku na kule. Harakaharaka alimsogelea ili kuhakikisha kama kweli amezinduka.

Alipohakikisha ni kweli, harakaharaka alitoka na kwenda kuwapa taarifa madaktari waliokuwepo muda huo, muda mfupi baadaye, kitanda chake kilikuwa kimezungukwa na madaktari wengi.

“Unajisikiaje binti?” aliuliza daktari Omondi huku akiwa makini kumpima Arianna vipimo mbalimbali, ikiwemo mapigo ya moyo. Msichana huyo alibaki kuduwaa kwani hakujua pale ni wapi na imekuwaje mpaka akafikishwa hapo. Kitu pekee alichokuwa anakumbuka ni kwamba alijidunga madawa ya kulevya kama kawaida yake lakini ghafla akaanza kusikia maumivu makali ya kichwa.

“Hapa ni wapi? Nimefikaje?” alihoji Arianna huku akijaribu kuinuka lakini maumivu makali ya kichwa pamoja na tumbo yalimrudisha kitandani, Dokta Omondi akamtaka kutulia watamueleza kila kitu kilichotokea.

Wakati madaktari wakiendelea kumhangaikia, Arianna alihisi hali isiyo ya kawaida tumboni kwake kutokana na jinsi tumbo lilivyokuwa linamuuma, alipojishika tu tumboni, aligundua kilichokuwa kimetokea lakini tofauti na madaktari walivyohisi kwamba huenda tukio hilo likamuumiza sana moyo wake, Arianna hakuonesha kabisa kujali.

Wakawa wanaendelea kuulizana maswali yaliyokosa majibu, wakahisi huenda bado madawa yalikuwa kichwani mwake na kusababisha akili yake isifanye kazi vizuri. Haikuwa kazi ngumu kumfikishia taarifa rasmi kwamba ujauzito wake umeharibika, kazi ya kumsafisha kizazi ikaanza huku akiendelea pia na matibabu ya kumaliza kabisa sumu ya madawa ya kulevya mwilini mwake.
***
Mechi ya kirafiki kati ya Msuya na Brianna ilianza lakini katika hali ambayo hakuwahi kuitegemea, Msuya alishangaa akikumbana na ukuta imara kwenye ngome ya msichana huyo ambaye naye alianza kulalamikia maumivu makali.

Msuya alibaki na maswali mengi yaliyokosa majibu lakini kwa sababu ndiyo kwanza mpambano ulikuwa unaanza na zilipita siku nyingi tangu alipoingia dimbani kwa mara ya mwisho, aliongeza kasi ya kukokota mpira, Brianna naye akazidi kuugulia maumivu makali.

Kutokana na hali aliyokuwa nayo Brianna, ilibidi Msuya asitishe mpambano muda mfupi baadaye kwani ilionesha hali ya mchezaji wa timu pinzani haikuwa nzuri na hakukuwa na uwezekano wa kurudi tena uwanjani lakini mpaka muda huo, tayari alikuwa amefanikiwa kuuvunja ukuta imara wa Brianna.

Alipoinuka na kwenda kuwasha taa, Msuya hakuyaamini macho yake kwa alichokiona, kitanda chote kilibadilika kabisa na kuwa kama machinjioni, huku akitetemeka alimsogelea Brianna ambaye alikuwa akiendelea kuugulia maumivu makali, akapiga magoti na kumuomba radhi kwa kilichotokea. Bado alikuwa akihisi huenda yupo kwenye njozi na muda mfupi baadaye atashtuka.

Msichana huyo hakujibu chochote zaidi ya kuendelea kugugumia kwa maumivu, akajikaza kisabuni na kusimama, akaanza kujikokota kuelekea bafuni, Msuya aliyekuwa bado amepiga magoti pale chini aliinuka na kutaka kumsaidia msichana huyo lakini alimsukuma kwa nguvu, akajikokota mpaka bafuni ambako alijifungia mlango kwa ndani na kuendelea kuugulia maumivu makali.

“Hivi nipo ndotoni au ni kweli?” alisema Msuya baada ya kuinuka pale alipokuwa ameangukia, akawa anafikicha macho yake na kujifinya lakini aligundua kwamba haikuwa ndoto bali kweli.

Alishindwa kuelewa nini kimetokea, mkewe ambaye alishakutana naye kimwili mara nyingi mpaka kumpa ujauzito ambaye baadaye uliharibika, leo amkute akiwa na usichana wake! Haikumuingia akilini.

Je, nini kitafuatia? Usikose Ijumaa kwenye Gazeti la Ijumaa.

1 Comment
  1. LICH says

    It look so nice

Leave A Reply