The House of Favourite Newspapers

The Angels of The Darkness (Malaika wa Giza)-70

0

Watoto wawili mapacha, Arianna na Brianna wanatenganishwa wakiwa bado wadogo kufuatia tukio baya la kigaidi linalotokea wakiwa mapumzikoni na wazazi wao nchini Kenya, kwenye kituo kikubwa cha biashara cha Kikuyu Mall jijini Nairobi.

Katika tukio hilo, baba wa watoto hao, Joseph Ndaki, Meneja wa Benki Kuu ya Tanzania, Tawi la Dar es Salaam na mkewe, Asia Mustafa wanapigwa risasi na magaidi hao na kupoteza maisha, wakiwaacha watoto wao wakiwa bado wachanga.
Kila mmoja anapitia maisha tofauti kabisa, Arianna anarejeshwa Tanzania wakati Brianna anaokotwa na mwanamke mwendawazimu, Mashango ambaye anaishi naye kwenye mtaa wa watu maskini jijini Nairobi uitwao Mathare.

Arianna anapata bahati ya kukutana na Msuya, mfanyabiashara mkubwa ambaye anampenda kwa dhati na kuamua kumuoa. Baadaye, Arianna ananasa ujauzito wa Diego na wanapanga njama za kutoroka.

Msichana huyo anafanikiwa kutorokea nchini Kenya, jambo linalomfanya Msuya atangaze dau nono.
Hatimaye, pacha wa Arianna, Brianna aliyekulia kwenye mitaa ya watu maskini Mathare, Nairobi nchini  Kenya anapatikana na kuchukua nafasi ya Arianna  lakini anaonesha tofauti kubwa ya kitabia, jambo linalomshangaza kila mtu.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…

Najua hujawahi kunywa pombe lakini leo nataka unywe huu mvinyo japo glasi moja tu, mwenyewe utafurahi,” alisema Msuya na kumbusu mkewe, kwa jinsi alivyokuwa na furaha, Brianna hakupinga, Msuya akafungua chupa moja na kumimina kwenye glasi mbili, wakaanza kunywa huku akimtazama mkewe kwa macho yaliyojaa matamanio.
Alipokunywa funda moja tu la mvinyo huo laini, Brianna alikunja uso kama anayesikilizia ladha yake, akashangaa kugundua kwamba haukuwa na ladha ya uchungu kama ambavyo amekuwa akisikia mara kwa mara kwamba pombe hazina ladha nzuri mdomoni.

Kutokana na ladha nzuri ya mvinyo huo, Brianna alijikuta akinogewa, akaendelea kunywa mpaka alipomaliza glasi nzima. Msuya akammiminia glasi nyingine, wakaendelea kunywa huku Brianna akizidi kubadilika kadiri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele.

Zile aibu zake za kikekike zikamuisha kabisa, akawa anachekacheka mwenyewe muda wote huku wakati mwingine akiongea mambo yasiyoeleweka. Msuya alikuwa akichekelea moyoni kwani alijua hatimaye anaenda kutimiza azma yake.
Kutokana na jinsi alivyokuwa amechangamka kutokana na mvinyo huo, hata Msuya alipoanza kumfanyia vitendo vya uchokozi wa kimapenzi, alikuwa akicheka tu. Msuya alienda kuwasha redio aliyoomba iandaliwe maalum kwa ajili ya kazi hiyo, akabonyeza kitufe kilichoandikwa ‘play’ kwenye redio hiyo.

Wimbo wa msanii mahiri wa Kimarekani, Marco Antonio Muñiz au maarufu kama Marc Anthony uitwao I Need You ulianza kusikika huku Msuya akifuatisha maneno yaliyokuwa kwenye wimbo huo:
“From the day that I met you girl, I knew that your love would be everything that I ever wanted in my life, from the moment you spoke my name, I knew everything had changed, because of you I felt my life would be complete… Oh baby I need you!”
(Tangu siku ya kwanza nilipokutana nawe, nilijua penzi lako ndiyo kitu pekee nilichokuwa nikikihitaji maishani mwangu, tangu kipindi ulipolitamka jina langu, nilijua kila kitu kimebadilika, kwa sababu yako nilihisi maisha yangu yamekamilika… Ooh mpenzi nakuhitaji!” aliimba Msuya kufuatisha wimbo huo huku akicheza taratibu kwa ustadi mkubwa, kitendo kilichomfurahisha mno Brianna, akawa anavunjika mbavu kwa kucheka. Huku akiendelea kucheza, Msuya alimfuata na kumshika mkono, akamuinua pale alipokuwa amekaa na kuanza kucheza naye.
Kwa kuwa tayari mvinyo ulikuwa ukifanya kazi kichwani, Brianna alianza kucheza ingawa hakuwa mahiri, wakaendelea kucheza huku msichana huyo akionesha kuwa na furaha iliyozidi kipimo.

Msuya akawa anaendelea kuonesha umahiri wake wa kucheza muziki wa taratibu, akamshika Brianna kiunoni na kumvutia kifuani kwake, wakawa wanaendelea kucheza taratibu huku mapigo ya moyo ya kila mmoja yakianza kubadilika.
Hata wimbo huo ulipoisha, walibaki wamesimama vilevile huku wakiwa wamekumbatiana kimahaba huku Brianna akipumua mithili ya mtu aliyetoka kukimbia mbio za mita mia moja.

Taratibu Msuya alimbeba kwenye mikono yake huku akimuangushia mvua ya mabusu, akaenda kumbwaga kwenye kitanda kikubwa kilichokuwa kimeandaliwa maalum kwa ajili ya wawili hao kisha na yeye akafuatia kwa juu. Akaendelea kumfanyia vituko vya hapa na pale vya kimahaba, msichana huyo akazidi kulegea.
Ile hofu aliyokuwa nayo kwa kipindi kirefu juu ya siri yake kujulikana, iliyeyuka kabisa, mvinyo aliokunywa ukampa ujasiri wa kuamua kwamba liwalo na liwe, akaanza kumuonesha ushirikiano Msuya, jambo lililomfurahisha mno mwanaume huyo.

Dakika kadhaa baadaye, wawili hao walikuwa kama walivyoletwa duniani, Msuya akajikuta akiwa kwenye hali mbaya zaidi kihisia kwani siku hiyo alimuona mkewe kama ameongezeka uzuri maradufu, maandalizi ya mchezo wa kirafiki usio na refa wala jezi yaliendelea na muda mfupi baadaye, kipyenga kilipulizwa kuashiria kuanza kwa mtanange huo.
Katika hali ambayo hakuwahi kuitegemea, Msuya alishangaa akikumbana na ukuta imara kwenye ngome ya msichana huyo ambaye naye alianza kulalamikia maumivu makali. Msuya alibaki na maswali mengi yaliyokosa majibu lakini kwa sababu ndiyo kwanza mpambano ulikuwa unaanza na zilipita siku nyingi tangu alipoingia dimbani kwa mara ya mwisho, aliongeza kasi ya kukokota mpira, Brianna naye akazidi kuugulia maumivu makali.
***
Manesi na madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya Mandera iliyopo kwenye Mji wa Mandera, jirani na mpaka kati ya Kenya na Somalia, waliendelea kuhaha huku na kule kujaribu kuokoa maisha ya mgonjwa aliyefikishwa hospitalini hapo muda mfupi uliopita, akiwa mahututi.

“Her blood pressure is extremely high and it has ruptured her blood vessels that is why she is bleeding.
There is a great probability she is going to start experiencing seizures in a short moment of time, there is extraordinary activities which is going on his central nervous system.”
(Shinikizo lake la damu ni kubwa sana kiasi cha kusababisha mishipa ya damu ipasuke ndiyo maana anatokwa na damu nyingi. Kuna uwezekano mkubwa muda mfupi baadaye akaanza kupatwa na kifafa, kuna hali isiyo ya kawaida inayoendelea kutokea kwenye mfumo wake wa fahamu) Dokta Faheem Omondi aliwaambia wenzake wakiwa ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi, wakijaribu kuokoa maisha ya Arianna.

“If that’s a case, we must administer her with Alprazolam Benzodiazepine intraveniously, also Nitroglycerin 0.5mg would be useful to dilates the blood vessels and takes some of the pressure off,”
(Kama ni hivyo, inabidi tumpe dawa ya kundi la Benzodiazepine iitwayo Alprazolam kupitia mishipa yake ya damu, pia tumpe Nitroglycerin 0.5mg kutanua mishipa ya damu na kushusha shinikizo la damu) alichangia daktari mwingine, wazo lililoungwa mkono na wote.

Harakaharaka akaunganishwa na mashine ya kumsaidia kupumua kisha akatundikiwa dripu za dawa na maji zilizoanza kutiririka kwa kasi kuingia kwenye mishipa yake ya damu.
“Why such a beautiful young lady like her is endangering her life by using drugs?” (Kwa nini msichana mdogo na mrembo kama huyu anahatarisha maisha yake kwa kutumia madawa ya kulevya?) madaktari walikuwa wakiulizana wakati wakiendelea kumhangaikia Arianna huku kukiwa hakuna dalili zozote za msichana huyo kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Je, nini kitafuatia? Usikose Jumatatu kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda.

SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

Leave A Reply