The House of Favourite Newspapers

Tigo Pesa Kibubu Yazidi Kuwanufaisha Wateja wa Tigo

0
Bi.  Mwanaidi Hussein Mwinyi (Mjasiriamali) Mwenye miaka 31 mkazi wa Kiyombo – Kitunda Dar Es Salaam.

 

 

BAADHI ya wateja wa Tigo Wameendelea kuisifia Huduma ya mfumo  wa Kidigitali wa Huduma za Kifedha kupitia simu za mkononi ambao unawawezesha wateja kuweka akiba ya kiwango fulani cha fedha za kielektroniki (e- money) na kujipatia riba kulingana na Kiwango cha fedha kilichohifadhiwa maarufu kama “TIGO PESA KIBUBU”.

Sehemu ya mifugo ya Bi. Mwanaidi.

 

 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti Bi.  Mwanaidi Hussein Mwinyi (Mjasiriamali) Mwenye miaka 31 mkazi wa Kiyombo – Kitunda Dar Es Salaam, Bwana Clementi Mvurungu (Mfugaji) Miaka 28 mkazi wa Kigoma , na Bwana Sokwe Matilio (Mjasiriamali) Miaka 36 mkazi wa Buza Dar Es Salaam wameelezea kwa jinsi gani Huduma ya Tigo Pesa Kibubu imeendelea kuboresha Maisha yao.

Kwa kuanza na Bi. Mwanaidi Mwinyi ameonyesha ni jinsi gani anaelekea kutimiza Ndoto yake ya kuwa Mfugaji Mashuhuri wa Kuku wa Kienyeji.

Bwana Clementi Mvurungu (Mfugaji) Miaka 28 mkazi wa Kigoma.

 

 

“Kwakweli nianze kwa kuwapongeza Tigo kwa kutuletea na maboresho wanayozidi kuyafanya katika huduma hii ya Tigo Pesa Kibubu, hadi sasa naendelea kuhifadhi pesa yangu kwenye akaunti yangu ya Tigo Pesa Kibubu na lengo langu ni kununua na kuanza kufuga kuku wengi wa kienyeji na naona ndoto yangu inaelekea kutimia maana nshaanza kununua kuku hao ambao baadhi yao ni Hawa unaowaona

Lakini pia mimi ni Mweka Hazina katika kikundi Chetu Kidogo cha VICOBA mimi na akina mama wenzangu na mimi kama mweka hazina nina jukumu la kuhakikisha kwamba pesa yetu ndogo tunayoipata inakua katika sehemu salama na sehemu iyo kwaupande wangu si nyingine bali ni TIGO PESA KIBUBU kwakweli nawapongeza sana Tigo kwa kutuletea na kuendelea kuboresha huduma hii maana kwanza naona naelekea kutimiza ndoto yangu ya kuwa mfugaji mashuhuri wa kuku wa kienyeji lakini pia imenijengea uaminifu kwa jamii yangu inayonizunguka
Alimalizia Bi. Mwanaidi.

Bwana Clement akiwajibika ujasiriamali katika masuala ya ufugaji.

 

 

Kwa upande wake Bwana Clement Mvurungu  mjasiriamali na mfugaji Mkazi wa Kigoma ameelezea furaha ya mafanikio aliyonayo ambayo yametokana na huduma ya Tigo Pesa Kibubu

“Mimi najivunia sana na nimefaidika na uwepo wa Huduma ya TIGO PESA KIBUBU maana mwanzoni wakati naanza kufuga nilianza na kuku nafikiri watano tu, lakini kadri siku zilivyokua zinazidi kusogea wale kuku walianza kutaga na kuatamia mayai mengi hapo ndipo nkaamua kujiongeza kwa kuweka akiba kwenye akaunti yangu ya TIGO PESA KIBUBU  ya kidogo nilichokua nkipata baada ya kuuza mayai na vifaranga, hadi mwishowe nikaongeza zaidi na kuanza kufunga bata , utaratibu wangu ulikua uleule hadi nilipofanikiwa kununua ng’ombe wawili na baadae watano lakini si hilo tu akiba yangu katika akaunti yangu ya TIGO PESA KIBUBU imenisaidia sana pale inapotokea dharula kwa mfano umeme unaponiishia usiku wa manane huwa naamishia akiba yangu kwenye akaunti ya Tigo pesa na kununua umeme alikadharika kwa dharura nyinginezo kama vile kulipia maji, kuwalipia wadogo zangu ada n.k.

Bwana Sokwe Matilio mkazi wa Buza Dar Es Salaam.

 

 

Naye Bwana Sokwe Matilio mkazi wa Buza Dar Es Salaam ameelezea kwa namna gani akaunti yake ya Tigo Pesa Kibubu imemsaidia Hadi sasa anaelekea kukamilisha ujenzi wa nyumba yake na mambo mengi kadha wa kadha

Kumbuka akaunti ya Tigo Pesa Kibubu itakuwa tofauti na akaunti yako kuu ya  Tigo Pesa.

Ni rahisi sana kuweka akiba kwenye akaunti yako ya  Tigo Pesa Kibubu, Piga *150*01#
Chagua Huduma za kifedha (7)
Chagua Akiba (8)
Chagua TigoPesa Kibubu (1)
Chagua weka akiba(1) na kisha weka kiasi na namba ya siri ya TigoPesa yako.

Kwa wateja wetu wanaotumia Tigo Pesa App, wanachotakiwa kufanya ni
Fungua Huduma za Kifedha
Chagua Akiba
Chagua Kibubu
Chagua kuweka akiba na kisha weka kiasi na  namba yako ya siri.

Huduma hii ni kwa kila mtumiaji wa Tigo Pesa, kuhamisha fedha kutoka Akaunti Kuu ya TigoPesa kwenda kwa Akaunti ya Kibubu ni BURE.

Leave A Reply