The House of Favourite Newspapers

Aliyekiri Kuua Watoto 14 na Kutoroka Mahabusu Auawa

0

MASTEN Wanjala mtuhumiwa aliye-make headlines kwa kukiri kuwaua zaidi ya watoto kumi na baadaye kutoroka katika kituo cha polisi alipokua anazuiliwa ameuawa na wananchi wa Bungoma Magharibi mwa Kenya.

 

Naibu Kamishena wa Kaunti ya Bungoma, Cornelius Nyaribai amethibitisha kifo chake katika ujumbe wa Twittter. Polisi wanasema Wanjala alifuatwa na wanakijiji hadi nyumbani alipokuwa katika Mji wa Bungoma na kupigwa hadi kuondoa uhai wake.

 

Mamlaka za usalama nchini humo zilikuwa zimeanzisha msako mkali kumtafuta mtu huyo ambaye alikiri kuwaua zaidi ya wavulana kumi katika kipindi cha miaka mitano. Masten Wanjala alitoroka katika mahabusu za polisi katika jijini Nairobi saa chache kabla ya kuitikia mashtaka ya mauaji ya wavulana 14.

 

Maafisa watatu wa Polisi wa Kenya waliokuwa kazini siku walifikishwa mahakamani siku ya Alhamisi na kufunguliwa mashtaka ya kumsaidia mtuhumiwa huyo. Wanjala alikamatwa mnamo Julai na alikiri kutumia dawa za kulevya na kuwaua wavulana wadogo, na pia kunywa damu zao katika visa vingine.

Leave A Reply