The House of Favourite Newspapers

Tigo Yaja na Mpya Sasa ni Kampeni ya Cha Asubuhi

0
Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Tigo, David Umoh.

Dar es Salaam, Jumanne, 15 Juni 2021 – Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania, leo imezindua kampeni mpya ya siku 90 inayoitwa Cha Asubuhi. Katika kampeni hii mpya kila mteja anayenunua kifurushi cha kila siku, kila wiki au kila mwezi atapata bonsai ya dakika za bure kupiga Tigo kwa Tigo kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi.

Mteja wa kifurushi cha kila siku atapata bonsai ya dakika 10 hadi mb 10, wakati mteja wa kifurushi cha kila wiki atapokea dakika 70 hadi mb 700 na mteja wa kifurushi cha kila mwezi atapata dakika 300 hadi GB 3.

Akizungumzia kampenihiyo, Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biasharawa  Tigo, David Umoh, alisema, “Daima tunatafuta njia za ubunifu za kuwazawadia wateja wetu wenye kazi na kuwafurahisha, kampeni hii inatoa fursa nzuri ya kuungana na wateja wote tuliokuwa nao kwa muda mrefu. ”

Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Biasharawa  Tigo, David Umoh (kushoto) akisisitiza jambo. Kulia ni Meneja Masoko wa Tigo William Mpinga. 

“Tunaamini kuwa mipango mingi hufanywa mapema asubuhi, na kwakuwa tuna nia ya kukidhi mahitaji ya wateja wetu kote nchini. Kampeni hii inawapafursa watu wanaoamka mapema na wale ambao wanapendelea kupanga shughuli zao za kila siku kuanzia asubuhi. ” alisema Umoh.

“Kwa miaka mingi Tigo Tanzania imekuwa ikianzisha ubunifu kama vile Facebook ya bure kwa Kiswahili, simu mahiriza Kiswahili na vifurushi kama tulivyofanya leo.

“Mipango yetu ni kuhakikisha tunaondoa vizuizi kwa wateja wetu kwaajili ya kufanya mawasiliano ya muhimu kupitia kampeni mpya ya Cha Asubuhi.

“Zaidi ya wateja milioni 12 wa Tigo wataweza kuamka na kupiga simu za bure, kuperuzi mtandao, bila wasiwasi wa kuwa na muda wa maongezi kwenye simu zao. Hii inadhihirisha juhudi zetu katika kuwa fursa inayowapa wateja wetu huduma bora, ” alisema Umoh.

Meneja Masoko wa Tigo akikisitiza jambo kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo.

Kampeni hiyo itaendelea kwa siku 90 na ipo kwaajili ya wateja wote wa Tigo.

Mteja anachotakiwa kufanya ni kununua kifurushi pendwa kupitia menyu ya USSD * 147 * 00 #, Tipo Pesa App au tavuti ya Tigo na kupata bonsai ya muda wa maongezi, bonsai ya data papo hapo, ambayo wanaweza kutumia kati ya saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi kwa kila siku bila malipo.

FURAHIA bonus za papohapo za dakika, SMS, pamoja na MBs/GBs za kumwaga kila wanaponunua kifurushi cha siku,wiki au mwezi.

Na kama haitoshi utaingia kwenye droo ya kushinda Samsung Note 20 na Simu Janja kibao ikiwemo Tecno Kitochi 4G Smart na Itel T20.

Unachotakiwa kufanya ni kununua kifurushi chochote cha siku, wiki au mwezi kwa Kupiga*147*00# pia kwa wateja wa Tigo Rusha na Tigo Pesa

Kila unapojaza Tunakujaza Tena! Vigezo na Masharti Kuzingatiwa

Asanteni Sana!

Leave A Reply