The House of Favourite Newspapers

Tigo Yazindua Wiki ya Huduma kwa Wateja 2022 Jijini Mwanza

0

Tigo Tanzania yazindua Wiki ya Huduma kwa Wateja 2022 jijini Mwanza. Sherehe hizo zitajumuisha shughuli mbalimbali zitakazo wanufaisha wateja wa Tigo. Tarehe 3, Oktoba 2022.

 

Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali nchini Tanzania, Tigo imezindua Wiki ya huduma kwa Wateja katika Mkoa wa Mwanza na baadaye katika maduka yote ya Tigo.

Maadhimisho hayo ya wiki nzima yanalenga kutambua thamani ya huduma na michango ya watoa huduma kwa wateja walio mstari wa mbele katika kuhakikisha wateja wa Tigo wanapata huduma bora nchini kote.

 

Katika nia ya kuimarisha utamaduni unaozingatia wateja na kuendana na mada ya mwaka huu; Sherehekea Huduma, watoa huduma walio mstari wa mbele kote nchini watasherehekea na kuungana tena na wateja katika safu ya shughuli zilizopangwa za wiki nzima.

Shughuli hizo ni pamoja na maonyesho, shughuli za ushiriki wa wateja, kutembelea soko ili kufanya vikao vya maoni. Zaidi ya hayo wateja watapata fursa ya kuzungumza moja kwa moja na watendaji wakuu wa Tigo katika kituo cha simu cha Tigo na maduka jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye duka la Tigo lililopo Rock City Mall jijini Mwanza, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Tigo, Mwangaza Matotola alisema.

 

“Kama kampuni ya mwasiliano ni muhimu kwetu kuelewa wateja wetu wanathamini nini, kwa upande mwingine sisi pia inabidi kuwapa pole watoa huduma wetu walio mstari wa mbele, Katika wiki hii uongozi wa Tigo utaungana na wafanyakazi wa kituo cha huduma ili kuwahudumia, kuwasiliana na kuwasikiliza wateja kwa lengo kuu la kuwathamini na kutafuta maoni kuhusu bidhaa na huduma zetu.”

 

Sherehe za wiki hii zitawafanya wateja wa Tigo kufurahia majaribio ya bure kwa baadhi ya huduma za kidijitali zilizochaguliwa, punguzo la bei kwa ununuzi wa vifaa vilivyochaguliwa vilivyounganishwa na intaneti ya BURE ya GB 8 kwa mwezi, pamoja na zawadi nyingi za bure katika maduka ya Tigo kote nchini.

 

“Kutoa huduma bora kwa wateja ni muhimu katika yote tunayofanya. Hili ni onyesho lingine la dhamira yetu ya kupendezesha maisha ya watoa huduma wetu walio mstari wa mbele, kama vile mada ya mwaka huu inavyodokeza” alisema Matotola.

Leave A Reply