The House of Favourite Newspapers

Tiwa Savage, mumewe Kurudiana?

0

TIWATiwa Savage

INAWEZEKANA! Baada ya kutabiri kupatana kwa ndugu wa damu ambao walikuwa hawapatani, Peter na Paul Okoye, staa wa vichekesho Nollywood, Ali Baba ametabiri tena staa wa muziki nchini humo, Tiwa Savage naye yupo mbioni kurudiana na mumewe, Tee Billz.

Pulse-Tee-Billz-Tiwa-Savage-JamilTiwa Savage na mumewe, Tee Billz.

Wengi wamekuwa wakichukulia utabiri wa Ali kuwa ni sehemu ya vituko lakini mara kwa mara anapokazania jambo hutokea na kuwa kweli.

ali-baba1-600x5961Staa wa vichekesho Nollywood, Ali Baba

Hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii, Ali aliandika; “Kama ningecheza kamari kuwa ndugu wa damu (P-Square) watarudiana…leo hii ningekuwa mshindi. Achana na hilo, nimetabiri kwa Tiwa tena, msishangae ila ukweli wako mbioni kurudiana, tutaona!”

Tiwa na Tee walifunga ndoa Novemba mwaka 2013 na kufanikiwa kupata mtoto mmoja, Jamil Balogun. Aprili mwaka huu walitengana huku kila mmoja akimtuhumu mwenzake kuwa msaliti.

Leave A Reply