The House of Favourite Newspapers

Tonombe, Niyonzima Watimka Yanga SC

0

KIUNGO mkabaji Mkongomani Mukoko Tonombe na kiungo mkabaji Mnyarwanda Haruna Niyonzima wameondoka kwenye kambi ya timu hiyo na kurejea majumbani kwao kwenda kuzitumikia timu zao za taifa.

Nyota hao pekee wa kimataifa walioitwa kwenye timu zao za taifa katika kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).

 

Tonombe hiyo ni mara yake ya kwanza kuitwa kwenye timu ya Taifa ya DR Congo tangu alipotua kujiunga na kikosi cha Yanga msimu huu akitokea AS Vita ambayo ilimuuza kwa dau la Sh 450Mil.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alisema kuwa wachezaji wao wawili pekee wa kimataifa Tonombe na Niyonzima hawapo kambini, wamerejea kwenye nchi zao kwa ajili ya kwenda kuzichezea timu za taifa.

 

Mwakalebela alisema kuwa, wachezaji hao wamewaruhusu juzi Jumatano baada ya kupokea barua kutoka kwenye mashirikisho ya soka ya nchi zao.

 

Aliongeza kuwa kiungo wao mshambuliaji Said Ntibanzokiza ‘Saido’ yeye yupo nyumbani kwao Burundi alipokwenda kwa ajili ya matibabu ya nyonga aliyoyapata akiwa katika majukumu ya klabu.

 

“Tonombe na Niyonzima hawapo kambini katika maandalizi ya kujiandaa na mchezo wetu wa ligi dhidi ya KMC ni baada ya kuwaruhusu kwenda kujiunga na timu zao za taifa.“

 

Tuliwaruhusu wachezaji hao baada kupokea barua za kuwaruhusu kutoka kwenye mashirikisho yao ya soka ya nchini kwao, hivyo uongozi ukachukua maamuzi ya kuwaruhusu kwenda kuzitumikia timu zao,” alisema Mwakalebela

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave A Reply