The House of Favourite Newspapers

Tonombe: Tulieni, Bado Mapambano Yanaendelea

0

KIUNGO Mkabaji wa Yanga, Mkongomani, Mukoko Tonombe, ameibuka na kutamka kuwa mapambano bado yanaendelea hadi mwisho wa msimu wawe mabingwa.Hiyo ni baada ya Yanga kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Jumamosi iliyopita.

 

Mkongomani huyo katika mchezo huo, alitolewa katika dakika za nyongeza baada kugongana na mchezaji wa Mtibwa wakiwania mpira.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Tonombe alisema amepata nafuu ya majeraha aliyoyapata katika mchezo huo, hivyo yupo fiti kwa ajili ya michezo ijayo.

 

Tonombe alisema kuwa baada ya kupona majeraha hayo akili na nguvu zake amezielekeza katika michezo ijayo ya ligi.

“Nianze kwa kuwashukuru mashabiki wote wa Yanga kwa maombi yao waliyonipa baada ya kupata majeraha katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa.“

 

Hivi sasa ninaendelea vizuri nashukuru bado tunaendela kupambana kuhakikisha tunafikia malengo yetu.“Kikubwa ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo wetu wa ligi, lakini siyo kazi nyepesi kikubwa tutaendelea kuipambania timu yetu,” alisema Tonombe.

Stori na Wilbert Molandi

Leave A Reply