The House of Favourite Newspapers

Travis Scott na Drake Washitakiwa kwa Vifo vya Mashabiki

0

MTU mmoja aliyehudhuria tamasha la Astroworld lililofanyika Ijumaa, Novemba 5, anayefahamika kama Kristian Paredes, amefungua kesi ya madai dhidi ya Rapa @travisscott na Drake juu ya vifo vya watu nane vilivyotokea Ijumaa wakati wasanii hao wakiwa wanapafomu.

 

Hayo yanakuja kufuatia vifo vya watu nane na majeruhi zaidi ya 300 waliohudhuria tamasha la Astroworld lililoanzishwa na Rapa Travis Scott tangu mwaka 2018, Kristian amefungua kesi hiyo ya madai kwa kile alichokiita kuwa ni uzembe wa wasanii hao wa kuchochea ghasia na vurugu ndiyo uliosababisha vifo hivyo.

 

Pia Kristian ametaka fidia zaidi ya shilling bilioni 2 kwa wote walioathiriwa na Tamasha hilo, huku akiwatupia lawama  wamiliki wa ukumbi na waandaaji wa Tamasha hilo juu ya usimamizi mbovu na ulinzi usioridhisha.

Cc; @bakarimahundu

Leave A Reply