Trump Athibitisha Marekani Kumuua Mtoto wa Osama

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amethibitisha kwamba Hamza Bin Laden mwana wa mwanzilishi wa kundi la Al Qaeda, Osama Bin Laden, aliuawa katika oparesheni iliyofanywa na  Marekani nchini Afghanistan.

 

Mwezi uliopita vyombo vya habari vya Marekani vilinukuu duru za kijasusi ambazo ziliripoti kwamba aliuawa katika shambulio la angani. Mtu huyo alyeitajwa na Marekani kuwa gaidi miaka miwili iliopita, alionekana kuwa mrithi wa moja wa moja wa baba’ke.

 

Akidaiwa kuwa na umri wa miaka 30, alikuwa ametoa wito wa mashambulizi dhidi ya Marekani na mataifa mengine.

”Hamza Bin Laden kiongozi mkuu wa Al-Qaeda na mwana wa Osama bin Laden aliuawa katika shambulio la oparesheni ya Marekani dhidi ya ugaidi nchini Afghanistan,” Trump alizungumza katika taarifa fupi iliyotolewa na Ikulu ya White House.

Taarifa hiyo haikueleza wakati operesheni hiyo ilipofanywa.


Loading...

Toa comment