TRUMP KUKUTANA TENA NA RAIS WA KOREA KASKAZINI

 

RAIS wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kwamba ataanda mkutano wa pili kujadili masuala ya nyuklia na kiongozi wa Korea ya Kaskazini mwezi huu.

 

Katika hotuba kwa taifa iliyoambatana na kauli mbiu “Choosing Greatness”, aliapa kwa mara nyingine kujenga ukuta katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico.

 

Huku akihimiza umoja, kiongozi huyo wa Republican pia amesema jitihada za ‘uchunguzi ulio na upendeleo’ wa Democratic huenda ukaathiri ustawi wa Marekani.  Hata hivyo, chama  cha Democrat kimemshutumu Trump kwa kupuuza maadili ya Marekani.

 

Hotuba hiyo imejiri baada ya pengo la muda mrefu kuwahi kushuhudiwa katika historia, la kusitishwa ufadhili kutoka serikali ya nchi hiyo.

 

Trump amesema atakutana na Kim Jong-un nchini Vietnam kuanzia Febrauri 27-28.

 

Mipango ya mkutano wa pili imekuwa ikipangwa tangu mazungumzo ya historia kati ya viongozi hao mwaka jana. Mkutano wa Trump na Kim mnamo Juni mwaka jana huko Singapore ulikuwa wa kwanza kati ya marais walio madarakani wa nchi hizo.

 

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment