The House of Favourite Newspapers

TUHUMA ZA KUPANGA MKAKATI DHIDI YA JPM, MEMBE AITWA CCM

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally amemtaka mwanachama wa chama hicho, Bernard Membe kufika ofisini kwake ili kutoa ufafanuzi wa tuhuma za kuandaa mpango wa kumkwamisha Rais John Magufuli.

 

Dkt. Bashiriu alitoa agizo hilo jana Ijumaa akiwa mkoani Geita kwenda kwa mwanadiplomasia huyo aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje na mgombea urais wa mwaka 2015. Bashiru alisema Membe anatuhumiwa kuandaa mipango hiyo kimyakimya na tangu ameteuliwa kushika wadhifa huo hajawahi kuonana na Membe.

 

“Kati ya wagombea wote wa CCM ni Membe peke yake ambaye sijakutana naye, namkaribisha ofisini, aje anieleze ninayoyasikia ni kweli au si kweli. Kwani haya yanayozungumzwa nyie hamyasikii? nasema peke yangu? Mimi ndiyo katibu mkuu wa CCM aje ajitetee kwamba yeye si kikwazo,” alisema Dk Bashiru.

 

“Iweje watu waseme kwamba wewe (Membe) unafanya vikao vya kutafuta kura za 2020, kwamba unataka kumkomesha Rais Magufuli, halafu unakaa kimya tu, sasa mimi nakualika uje ofisini kama ni mwanachama wa kweli aliyetoa ahadi ya uanachama wa CCM ya kusema kweli daima fitina kwangu mwiko njoo ofisini ueleze,” ameongeza.

 

Kwa upande wake Membe amejibu na kusema haya;

“Usiku huu nimempelekea Katibu Mkuu wa chama chetu Ndg. Bashiru ujumbe wa kukubali kumwona mara nitakaporejea kutoka nje ya nchi. Nimeshangazwa kidogo na utaratibu uliotumika kuniita, sababu ya ugeni kazini na kwa sababu ninamheshimu nitakwenda kumwona ofisini kwake.

 

“Tuhuma nitungiwe Mimi alafu nipangiwe na kujibu. Nimemwomba Katibu Mkuu siku nitakayokwenda kumwona, Musiba awepo ili atoe ushahidi kwa sababu mtoa tuhuma ndiye mwenye wajibu wa kuthibitisha aliyoyasema,” amesema Membe.

MAGUFULI ‘Alivyomuita’ MWAKYEMBE Hadharani, Kampa Maagizo Haya!

                                   

Comments are closed.