The House of Favourite Newspapers

Tumia mayonnaise kuzijaza nywele zako

0

e76288c0-5f9d-4fb0-866e-d3d91d7e2d50._CB317083109_Wiki hii kwenye safu ya urembo tutaongelea jinsi ya kujaza nywele kwa kutumia mayonnaise hasa kwa wale wenye nywele zinazokatika mbele.

Unafanyaje?
Osha nywele zako kwa shampoo nzuri ambayo unajua haikati nywele, baada ya hapo usizikaushe zikiwa na maji bado zipake mayonnaise kuanzia chini kwenye ngozi kisha zichanganye nywele zote.
Acha kwa muda wa dakika 15 kisha osha kwa kutumia maji na shampoo tena.
Mayonnaise ina uwezo mkubwa wa kuotesha nywele zako zinazokatika lakini pia ina uwezo wa kujaza nywele ambazo ni chache kichwani.
Kama utafanikiwa kupata kwa wingi tumia kwa wiki mara mbili utafurahia ujazo wa nywele zako.

Nyongeza
Tumia ice cream kulinda ngozi yako ya macho.
Hivi unajua kuwa unaweza kutumia ice cream ili kulinda ngozi ya macho yako? Kama hujui, habari ndiyo hiyo.
Mara nyingi ukiamka umechoka unaweza kujikuta unapata weusi chini ya macho ambao si wa kawaida hii inamaanisha ngozi imechoka. Cha kufanya ni kuchukua ice cream ya maziwa tu bila fleva, paka chini ya macho na kuzunguko jicho lako lote.
Ice cream huwa inasaidia kuituliza ngozi na wakati mwingine kuifanya iteleze na kuwa nyororo.

Leave A Reply