The House of Favourite Newspapers

Tundu Lissu Apelekwa Nairobi Kutibiwa

0
Tundu Lissu akipandishwa kwenye ndege.

MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameondoka katika uwanja wa ndege wa Dodoma usiku huu kwenda Nairobi kwa ajili ya matibabu.


Lissu ambaye alijeruhiwa akiwa kwenye gari nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulika.


Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini amesema, katika safari hiyo Lissu ameambatana na mkewe, madaktari wawili wasio na mipaka, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.


Selasini amesema kuwa Lissu anapelekwa katika Hospitali ya Aga Khan mjini Nairobi. Ndege hiyo iliyombeba ya 5H-ETG imeondoka katika Uwanja wa Dodoma saa sita na robo usiku.

Aidha, Katibu wa Wabunge wa Chadema, David Silinde amesema kuwa wabunge wa chama hicho wameamua kuchangisha fedha kwa ajili ya kufanikisha kumsafirisha Lissu kwenda Nairobi kutibiwa.

Leave A Reply