The House of Favourite Newspapers

Tundu Lissu Awasili Ubelgiji Kwa Ajili Ya Matibabu Ya Mazoezi Ya Viungo

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu akiwa na madaktari baada ya kufika Ubelgiji.

 

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amewasili katika uwanja wa ndege jijini Brussels, nchini Ubelgiji ambapo amepelekwa kwa ajili ya awamu ya tatu ya matibabu yake yatakayohusisha mazoezi ya viungo.

Tundu Lissu amewasili jijini hapo akitokea katika Hospitali ya Nairobi, nchini Kenya alikokuwa anapatiwa matibabu kwa muda wa takribani miezi minne sasa kutokana na kushambuliwa kwa risasi mnamo septemba mwaka jana mkoani Dodoma


Mbunge Tundu Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa akitoka Bungeni, majira ya saa 7 mchana, karibu na nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma.


Kwa mujibu wa taarifa ya madaktari waliokuwa wanamtibu, walieleza kuwa jumla ya risasi 16 zilimpata Tundu Lissu mwilini mwake na wamefanikiwa kuzitoa 15, isipokuwa moja ambayo ipo nyuma ya uti wa mgongo.
Tundu Lissu alieleza kuwa wataalamu na madaktari wake walishauri risasi hiyo ni hatari zaidi kama ikitolewa kuliko ikibaki ndani ya mwili wake kutokana na eneo ilipokwama.


Comments are closed.