The House of Favourite Newspapers

TUZO MCHEZAJI BORA VPL LEO NI LEO

 

Emmanuel Okwi.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), leo Jumamosi linatarajiwa kutoa tuzo mbalimbali kwa wale waliofanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/2018, katika sherehe zitakazofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.

 

Mchakato wa kufunga upigaji kura uliowahusisha makocha, manahodha wa timu za ligi kuu na Wahariri wa Habari za Michezo, ulifungwa Jumatano iliyopita.

Wachezaji watatu watakaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara ni Emmanuel Okwi, John Bocco na Erasto Nyoni ambao wote wanaichezea Simba.

 

Jumla ya tuzo 16 zinatarajiwa kutolewa leo ambapo baadhi ni za kikanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo tayari washindi wake wamefahamika, nazo ni bingwa, mshindi wa pili, mshindi wa tatu, mshindi wa nne na mfungaji bora.

 

Pia kutakuwa na tuzo nyingine mbalimbali ikiwemo za timu yenye nidhamu inayowaniwa na Kagera Sugar, Simba na Mtibwa Sugar, wakati Mchezaji Bora Chipukizi ikiwaniwa na Shaaban Idd Chilunda, Yahya Zayd (Azam) na Habibu Kyombo (Mbao), mwamuzi bora, bao bora, kipa bora na kocha bora.

Comments are closed.