The House of Favourite Newspapers

TUZO ZA SZIFF 2019… Filamu za Globa TV Zapasua

Maseke

LAZIMA kieleweke! Unaweza sema hivyo kwa lugha nyepesi baada ya kufunguliwa kwa mara nyingine pazia la kupiga kura kwa Tuzo za Sinema Zetu nchini zijulikanazo kama Sinema Zetu International Film Festival (Sziff) ambapo hadi sasa zoezi la upigaji kura limefikia pazuri.

 

Katika tuzo hizo, filamu tatu zinazorushwa kupitia Global TV Online ambazo ni Chanzo ni Wewe, Ardhi ya Damu na Coretha zimeingia katika vinyang’anyiro mbalimbali.

Akizungumza na Risasi Vibes, mmoja wa washiriki wa filamu hizo kupitia Filamu ya Ardhi ya Damu, Sango Johannes alisema kuwa, tangu kufunguliwa zoezi la upigaji kura katika tuzo hizo wengi wamejitokeza.

 

GLOBAL MOVIES: CORETHA (PART TWO)

“Tunaweza kusema tumefikia pazuri kutokana na uhamasishaji unaoendelea na vilevile mashabiki wengi kujitokeza. Kwa siku tunaweza kupata simu hadi 50 wengine wakiomba maelekezo zaidi ya kupiga kura na wengine wakijitoa kuwahamasisha wengine ambao hawajapiga.

 

Rhoida

 

“Kumbuka unaweza kupiga kura mara nyingi uwezavyo kwa kufuata tu njia zinazotakiwa, ni jambo la kuwa na simu yako ya mikononi tu,” alisema Johannes.

Jinsi ya kupiga kura, ingia sehemu ya kuandika meseji kwenye simu yako.

Magreth.

 

Kwa msanii Bora wa Kiume, andika BM kisha acha nafasi andika 1000, acha nafasi na uandike *8 kisha tuma kwenda namba 0683 520 006 hapo utakuwa umempigia kura Emmanuel Maasa aliyecheza Filamu ya Coretha.

 

GLOBAL MOVIES: CORETHA (PART ONE)

 

Msanii Bora wa Kike, Rhoida andika BF acha nafasi kisha andika 760, acha tena nafasi andika *9 na utume kwenda 0683 520 006.

Kwa Filamu Bora ya Mwaka kupitia Filamu ya Ardhi ya Damu andika 760 kisha acha nafasi, andika *9 na tuma kwenda 0683 520 006.

 

Surej

 

Filamu ya Chanzo ni Wewe andika 360 kisha acha nafasi, andika *7 na utume kwenda 0683 520 006.

Filamu ya Coretha andika 1000 kisha acha nafasi, andika *8 na utume kwenda 0683 520 006.

Kilele cha tuzo hizi ambazo huandaliwa na kituo cha TV cha Azam kupitia chaneli yao ya Sinema Zetu, kinatarajiwa kufanyika kuanzia Februari 23, mwaka huu.

Risasi VIBES.

 

GLOBAL MOVIES: CHANZO NI WEWE (PART ONE)

 

 

Comments are closed.