The House of Favourite Newspapers

Twitter Kufuta Wafuasi wa Trump Kabla ya Kumkabidhi Biden

0

TWITTER  imethibitisha kwamba mamilioni ya wafuasi wa akaunti rasmi ya Rais wa Marekani watafutwa kabla ya akaunti hiyo kukabidhiwa utawala wa Rais Mteule, Joe Biden.

Timu ya  Biden ilipinga mpango huo  lakini kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii ilisema kwamba uamuzi wake ‘haubadiliki’.

Hatua hiyo inaashiria mabadiliko kutoka kwa utawala unaoondoka. Twitter ilikubali ombi la  Trump 2016 kuwarithi mamilioni ya wafuasi wa Barack Obama.

”Mwaka 2016, utawala wa Trump uliwarithi wafuasi wote wa Obama katika akaunti ya @POTUS na ile ya @Whitehouse”, Rob Flaherty, mkurugenzi wa masuala ya mtandaoni alisema katika ujumbe wake wa Twitter siku ya Jumatatu.

”Mwaka 2020 , Twitter ilituarifu kwamba utawala wa  Biden utalazimika kuanzia sifuri”.   Inaathiri wafuasi wa akaunti zinazomilikiwa na serikali kama vile @POTUS na @FLOTUS.

Twitter ilisema kwamba wale wanaomfuata rais aliyepo madarakani wataarifiwa kwamba wanawekwa katika kumbukumbu na watapatiwa chaguo la kufuata akaunti ya utawala mpya wa Biden.

Akaunti ya kibinfasi ya  Biden @Joe Biden , ina wafuasi milioni 21.7 na haitaathiriwa na hatua hiyo mpya.

Rais Trump amekuwa akitumia akaunti zake za Twitter rasmi na kibinafsi kuzungumza na wapigaji kura. Wakati wa utawala wake  Ikulu  amechapisha zaidi ya ujumbe 50,000.

Hata hivyo, ukweli ni kwamba tovuti inayofuatilia ujumbe wa Twitter na akaunti za wafuasi tangu mwezi Novemba, inasema kwamba  Trump alipoteza wafuasi 369,849 katika akaunti yake binafasi tangu mwezi Novemba.

Wakati huohuo,  Biden amejiongezea wafuasi 2,671,790. Hatua hiyo kutoka Twitter inajiri siku chache baada ya afisa mkuu mtendaji, Jack Dorsey, kuondoa ufuasi wake kwa  Trump, Biden na Makamu wa Rais Mteule, Kamala Harris.

Mtaalamu wa masuala ya soko, Rebecca Lodge, kutoka kampuni ya Start Up Disruptors alisema kuhusu uamuzi huo wa Twitter: Huku mamilioni ya watu wakiwa wafuasi wa akaunti moja mbali na kwamba wafuasi wa Donald Trump wana ushabiki mkubwa wa kiongozi huyo, huenda ni mpango wa Twitter kuhakikisha kwamba jumbe zozote zenye nia mbaya zinapunguzwa makali kabla ya rais mpya kuchukua mamlaka.

Leave A Reply