The House of Favourite Newspapers

Ubia wa TTCL na Bharti Airtel Wafikia Kikomo

0

Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (wa kwanza kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Profesa Tolly Mbwete (katikati) hati ya mauzo ya hisa asilimia 35 za Kampuni ya Bharti Airtel Afrika. Serikali imezinunua rasmi hisa za kampuni hiyo ndani ya TTCL ambapo leo wamesaini mkataba wa mauziano wa hisa hizo. Kulia ni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria akishuhudia.

Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (mwenye tai ya bluu) akionesha hati ya mauziano ya hisa. Serikali leo imezinunua rasmi hisa asilimia 35 za kampuni ya Bharti Airtel Afrika ndani ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), ambapo sasa inakuwa ikiimiliki TTCL kwa asilimia 100. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria (mwenye tai nyekundu) akiwa kwenye hafla ya kusaini mkataba wa mauziano hayo.  Nyuma waliosimama ni viongozi mbalimbali wa TTCL na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano walioshuhudia tukio hilo.
Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (kushoto) akibadilisha hati ya mkataba wa mauziano ya hisa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali walioshuhudia tukio hilo.
Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (mwenye tai ya bluu) akionesha hati ya mauziano ya hisa. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria (mwenye tai nyekundu). Kulia ni Ofisa Mkuu Mdhibiti wa Kampuni ya Bhart Airtel Afrika, Daddy Mukadi akiwa kwenye hafla hiyo.
Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (katikati) akizungumza katika hafla ya kutiliana saini ya mauziano ya hisa. Serikali leo imezinunua rasmi hisa za Kampuni ya Bharti Airtel Afrika. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Maria Sasabo akiwa katika hafla hiyo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura (wa kwanza kulia).

Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (kushoto) akijadiliana jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria kwenye hafla ya kutiliana saini ya mauzo ya hisa asilimia 35 za kampuni ya Bharti Airtel leo Dar es Salaam.

Serikali kufanya marekebisho ya Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kieletroniki ili kuwezesha watanzania kumiliki hisa zitakazouzwa na Kampuni za Mawasiliano kupitia soko la hisa.
Hayo yamesemwa leo Bungeni  Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Pichani)alipokuwa akiwasilisha Bungeni  muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2016.
“Mhe. Naibu Spika, sehemu ya nne inapendekeza marekebisho katika sheria ya Posta na   Mawasiliano ya Kielektroniki, sura 306 kama ifuatavyo, kufuta kifungu cha 6(2d) na kukiandika upya ili kuweka sharti kwa kampuni za mawasiliano kuwasilisha Katiba ya Kampuni itakayothibitisha muundo wa umiliki wa hisa kama mojawapo ya taarifa zinazopaswa kuwasilishwa wakati wakuomba leseni,” alifafanua Mhe. Mpango.
Aidha Mhe. Mpango aliendelea kwa kusema kwamba, watoa huduma za Mawasiliano ya Kielektroniki watawekewa sharti la kuuza hisa zao kwa Umma na kusajili hisa zao katika soko la hisa Nchini Tanzania ili kutoa fursa kwa watanzaniai kununua hisa na kumiliki asilimia 25 ya Kampuni hizo.
Kutokana na marekebisho ya sheria hiyo, kampuni za huduma za Mawasiliano ya kielektroniki ambazo tayari zimesajiliwa hapa Nchini zitawajibika kujioredhesha katika soko la hisa na kuuza hisa zao ndani ya kipindi cha miezi sita kuanzia Julai 01, 2016.
Vile vile kampuni ambazo zitasajiliwa baada ya Julai 01, 2016 zitawajibika kuuza hisa zao na kujioredheshsha katika soko la hisa ndani ya kipindi cha Miaka miwili kuanzia Julai 01, 2016.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti  Mhe. Hawa Ghasia amesema kwamba kamati imekubaliana na marekebisho hayo aidha kamati inaishauri Serikali  kuweka tafsiri ya watanzania ili kuwezesha hisa hizo kuuzwa kwa watanzania  pekee na pia kuangalia suala la miezi sita kwa makampuni yaliyosajiliwa lisilete utata kwenye utekelezaji wake.
Leave A Reply