The House of Favourite Newspapers

Ubingwa wa Global TV… Mabondia watambulishwa, Tayari kwa Vita

0
Idd Pialali wa Tanzania (kushoto) na Regin Champion wa Congo wakitambiana.

 

KAMISHENI ya ngumi za kulipwa leo umewatambulishwa mabondia wote wanaotarajia kupanda ulingoni Julai 22, mwaka huu katika pambano ya kimataifa y ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati yatafanyika kwenye Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem, Dar huku yakirushwa mubashara  kupitia kituo cha Global TV.

 

Mabondia hao ambao wametambulishwa na rais wa kamisheni hiyo, Yassin Abdallah ‘Ustaadh’ ambao ni Franci Miyeyusho ‘Chichi Mawe’, Nasibu Ramadhan ‘Pacman’ Idd Pialali huku kwa upande wa wageni kutoka nje akiwa ni Israel Kamwamba wa Malawi na Regin Champion kutoka  nchini DR Congo.

 

Rais wa kamisheni hiyo, Yassin Abdallah ‘Ustaadh’ akiwatambulisha Idd Pialali (kushoto) na Regin Champion.

 

Katika utambulisho huo Ustaadh alisema kuwa Mtanzania Francis Miyeyusho atazichapa na Israel Kamwamba, Idd Pialali dhidi Regin Champion wakati Nasibu Ramadhan akitarajia kucheza na Mzambia, Benard Mwango badala ya Mzimbabwe, Tinashe Mwadziwana aliumia wakati wakiwa mazoezini.

 

Niwambie mashabiki wa ngumi kuwa tayari mabondia wameshaingia kwa ajili  ya maandalizi ya mwisho kabla ya kufanyika kwa pambano lenyewe na kikubwa balozi wa Malawi, Hawa Ndilowe amekubali kuwa mgeni wa heshima na tunamuomba mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro  akubali kuungana nasi siku hiyo  kwa sababu ndiyo mlezi wa ngumi za kulipwa.

 

Akimtambulisha Israel Kamwamba

“Lakini  hili pambano limedhaminiwa Global TV na watarusha mubashara kupitia kupitia website yake ya www.globaltvtz.com kwa sababu mashabiki watakaopata fursa ya kuingia watakuwa na kadi maalum za mwaliko hivyo wengine wataona bure kabisa kupitia kituo hicho,” alisema Ustaadh.

Katika hatua nyingine, pambano hilo, hakutakuwa na kiingilio na mashabiki wataweza kulishuhudia mubashara kupitia simu zao za mkononi kwani litaoneshwa na Global TV pekee. Wadau na mashabiki watakaopata nafasi ya kuingia ukumbini wataingia kwa kadi maalum za mwaliko.

 

Israel Kamwamba akitunisha msuli.

 

Ili kulishuhudia pambano hilo kwa njia ya simu tena bure, hakikisha unajiunga (SUBSCRIBE) na YouTube Channel ya Global TV Online sasa hivi ili usipitwe. Ingia YouTube, tafuta GLOBAL TV ONLINE, kisha bonyeza neno SUBSCRIBE pia bonyeza kikengele kidogo kilichopo pembeni yake ambacho kitakukumbusha kuangalia pambano hilo mara tu litakapoanza.

Kama wewe umeshajiunga, basi hakikisha pia umebonyeza kikengele ili usipitwe na kila kinachoendelea Global TV. Pia unaweza kutupata kupitia mtandao wa www.globaltvtz. com, jiunge sasa na Global TV ili uwe wa kwanza kuona ndondi za kimataifa. Kajiunge sasa kwa kuingia www.youtube.com/user/ uwazii.

 

IBRAHIM MUSSA |  GLOBAL PUBLISHERS

 

Leave A Reply