The House of Favourite Newspapers

Uchaguzi wa Rais Algeria, Wasiwasi Watanda

0

WANANCHI wa Algeria wameendelea kuandamana katika miji mbalimbali nchini humo wakidai mageuzi kamili ya mfumo wa kisiasa nchini mwao na kupinga uchaguzi wa rais ambao unafanyika leo Alhamisi, Desemba 12, 2019.

Jeshi la taifa lenye ushawishi mkubwa katika siasa za Algeria halimuungi mkono mgombea yeyote katika juhudi za kuwahakikishia wananchi kwamba uchaguzi utakuwa huru na wa haki.

 

Maandamano makubwa yametokea nchini Algeria tangu mwezi April walipomlazimisha aliyekuwa Rais wa taifa hilo Abdelaziz Bouteflika kwa miaka 20 kujiuzulu nafasi hiyo.

Leave A Reply