The House of Favourite Newspapers

Uchumba wa Linah wavunjika

1

linah Staa wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’.

Na Musa Mateja
CHALII! Lile penzi lililoshika kasi kama moto wa kifuu kati ya staa wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ na William Bugeme ambaye ni kaka wa kufikia wa Zarinah Hassani ‘Zari The Boss Lady’, limevunjika na sasa kila mtu amechukua hamsini zake.

Linah-444Estelina Sanga ‘Linah’ na William Bugeme akiwa na mpenzi wake huyo.

Akizungumza na mwanahabari wetu hivi karibuni, Linah aliweka wazi kwamba msingi wa penzi lao lilivyokuwa wanaujua wenyewe hivyo wamefikia hatua ya kulivunja na hakuna sababu ya watu kuwachimbachimba kila kukicha, ieleweke kuwa kwa sasa kila mmoja yupo kivyake.

“Mimi na William kwa sasa hatuko pamoja hivyo naomba tu watu waniache maana kila kukicha wamekuwa wakiropoka wanavyovijua wao, nilikuwa na William kwa kipindi fulani, tumeshamalizana hivyo kila mmoja anafanya yake, sioni sababu ya watu kuhoji juu ya suala hili zaidi naomba tu watambue kwamba hakuna chenye mwanzo kisichokuwa na mwisho,” alisema Linah.

Wawili hao walianzisha uhusiano miezi mitano iliyopita lakini kwa sababu ambazo Linah ameziita kuwa ni za binafsi, wameamua kumwagana na sasa kila mmoja anaendelea na michakato yake.

1 Comment
  1. Prince'otto Kabagala says

    Njoo kwangu nkutunze Linah. Mimi ntakujali!

Leave A Reply