The House of Favourite Newspapers

Malaika akataa kolabo

0

6B3A3875Msanii wa Kizazi Kipya, Diana Exavery ‘Malaika’.

NA gladness mallya
MWANADADA anayefanya vizuri kwenye Muziki wa Kizazi Kipya, Diana Exavery ‘Malaika’ amesema kwa sasa hayupo tayari kufanya kazi kwa kushirikiana (kolabo) na mwimbaji wa kike, kwa kile alichosema, hajajipanga.

Akizungumza na gazeti hili juzikati, Malaika alisema anafanya hivyo kwa vile anahitaji kazi yake ya sasa ifanye vizuri na kufahamika, kabla ya kufikiria kufanya kazi, hasa na msanii mwanamke.

“Kwa sasa naipa nafasi ngoma yangu mpya ya Zogo mpaka mwakani ndipo nitapanga kufanya kazi nyingine, sina mpango wa kufanya kolabo na msanii wa kike kwani sina wimbo wa kumshirikisha mtu ila siku ikitokea nitawashirikisha,” alisema Malaika.

Leave A Reply