The House of Favourite Newspapers

Uchumba wa Wolper ni Aibu ya Milele!

0

KUNA kipindi kinafika haya maisha tuliyonayo sasa hatutakuwa nayo tena hapo baadaye. Kuna umri unafika, unapoteza kabisa mvuto ulionao sasa. Unakuwa huna uwezo tena wa kupambana na maisha kama ulivyo sasa.

 

Hicho kipindi unakuwa huwezi tena kucheza na wanaume kama unavyocheza sasa. Ndiyo maana wahenga wakasema, mbio za sakafuni huishia ukingoni.

 

Huu ndio wakati wa kijana kutengeneza maisha yake ya baadaye kwa kutumia njia sahihi na zinazofaa kwa jamii ili baadaye zisije kukuletea madhara.

Leo nimeona niongee kidogo na mrembo anayefanya poa kunako gemu ya filamu Bongo. Si mwingine, namzungumzia Jacqueline Wolper Massawe.

 

Ndiyo, ni mrembo hasa kwa sababu kwa macho ya nje, mashaallah, Mwenyezi Mungu kamjaalia kwelikweli.

 

Mtoto ana rangi ya chungwa, urefu wa twiga, mguu sasa ndiyo balaa, watoto wa mjini wanasema ana mguu wa bia, hicho kisura chake ndiyo usiseme, kwenye suala la utafutaji, nako hajaachwa nyuma, ni mwanamke mpambanaji sana, lakini hivi vyote akivitumia vibaya, kuna siku atajutia.

Kama unakumbuka vizuri, utagundua kuwa mwanadada huyu aliingia kwenye gemu mwaka 2007 na moja ya muvi alizowahi kucheza ni pamoja na Family Tears, Tom Boy, Dereva Taxi na nyingine nyingi, zilizofanya vizuri sokoni na watu kumjua zaidi.

 

Tangu mwaka huo mpaka sasa, jina lake ni kubwa kiasi kwamba huwezi ukataja listi ya mastaa wanaofanya vizuri kwenye filamu bila kutaja jina lake.

 

Miaka kadhaa iliyopita mpaka sasa, Wolper ameshahusishwa kimapenzi na wanaume wengi, huku waliojitokeza kumvisha pete wakiwa wanne ambao ni Abdallah Mtoro ‘Dallas’ Putin ‘Mkongo wa Wolper’ Sadick Athanas ‘Engine’ na Rashid ‘Chidy Design’ aliyemvisha wiki iliyopita, lakini kabla hata ya wiki kupita, wawili hao tayari wameshaachana.

 

Lengo la kuandika mambo yote haya ni kutaka kumkumbusha bishosti huyu kwamba umri unakwenda na siku hazigandi, Desemba 6, mwaka huu atafikisha miaka 33 kamili.

Hivyo basi, akiendelea kucheza na maisha yake sasa hivi, atajikuta anazeeka bila kuwa na familia.

 

Kitendo cha kuvishwa pete na wanaume tofauti bila kuwa na ndoa, kwako ni aibu ya milele. Ni ya milele maana, pete hizi hata iweje, zinabaki kwenye mitandao kama Google, YouTube na mingine na vizazi na vizazi vitashuhudia matukio haya.

 

AJIHESHIMU

Katika vitu ambavyo mwanadada huyu anatakiwa kuvizingatia hasa kwa kipindi hiki ni kuhakikisha anajiheshimu na kuwaheshimu wengine. Asiruhusu watu wakamuongelea mambo ambayo yanazidi kulichafua jina lake.

 

Wolper amekuwa na sifa mbaya ya kuhusishwa kimapenzi na vijana wadogo ambao pengine angewahi kuzaa, angeweza kuwazaa. Miezi kadhaa iliyopita alihusishwa kimapenzi na msanii wa Hip Hop Bongo, Young Killer ambapo licha ya kila mtu kumsema bishosti huyo kuwa kwa nini anatoka kimapenzi na watoto wadogo, maneno yao hayakuzaa matunda.

 

Kwani mwisho wa siku watu walitulia na kumuacha aendelee na maisha yake, hatukukaa sawa hivi karibuni baada ya kuvalishwa pete, msanii wa Singeli; Meja Kunta naye akaibuka na kudai kuwa amewahi kutoka kimapenzi na mrembo huyo, bibie unakwama wapi?

 

Kwa nini kuwang’ang’ania hawa vijana wadogo ambao siyo saizi yako? Kwa nini usiige mifano kutoka kwa wasanii wenzio kama akina Rose Ndauka, Esha Buheti, Chuchu Hans na wengine? Mbona wao wanafurahia maisha yao na wala hatuwaoni mitandaoni wakisakamwa na maneno ya shombo kama wewe?

 

Ukijiheshimu na kujitunza, nina imani utapata mwanaume mzuri sana ambaye mtaendana, kwa sababu wewe ni mwanamke mzuri na umekamilika, achana na mambo ya kuwaruhusu hao vijana wachezee maisha yako.

 

Ona mpaka sasa umeshavalishwa pete ya uchumba na wanaume wanne tofauti na wote kati yao hakuna hata mmoja aliyetangaza ndoa, daah! Huoni kama wanakuharibia sifa yako hata kama kuna mwanaume yupo siriazi anahitaji kukuoa ataogopa kutokana na skendo na idadi hiyo ya wanaume uliyonayo?

 

Kama ni kiki hazikusaidii kitu, hizi zinazidi kuharibu jina lako. Umeshakuwa mtu mzima, tulia utapata mwanaume sahihi kwenye maisha yako, atakayekupenda kwa dhati na kuvumilia mapungufu yako yote uliyo nayo.

MAKALA: MEMORISE RICHARD, BONGO

Leave A Reply