The House of Favourite Newspapers

Ufunguzi Ndondo Cup 2017… Makuburi FC Vs Stim Tosha Zatoshana Nguvu

0
Line up ya Makuburi FC

LEO Jumamosi Juni 17 zilikuwa shamra shamra za uzinduzi wa michuano ya soka la mitaani maarufu kama Ndondo Cup 2017 ambazo zimefanyika katika Uwanja wa Kinesi uliyopo Shekilango, Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo mashabiki kibao wamejitokeza kushuhudia uzinduzi huo.

Line up ya Stim Tosha

Katika uzinduzi huo, timu za Makuburi FC yenye maskani yake mtaa wa Makuburi na Stim Tosha zilishuka dimbani kumenyana vikali ambapo mchezo huo ulikuwa wa kuvutia na wenye upinzani wa aina yake.

Msanii wa muziki wa Singeli (kushoto), Sholo Mwamba akimsalimia Mwenyekiti wa Yanga wa zamani, Imani Madega uwanjani hapo.

Mashabiki wa timu zote mbili walionekana kuzisapoti timu zao mwanzo mwisho huku mbwembwe za mitaani zikichukua nafasi uwanjani hapo. Michezo mbalimbali, utani wa kiganga na kelele za kushangili ndivyo vilitawala muda wote wa mchezo huo.

Sholo Mwamba akimsalimia msanii mwenzake, Hamad Ally ‘Madee’

Mastaa kibao waliibuka uwanjani hapo kushuhudia game hiyo wakiwemo, wanamuziki na wachezaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na viongozi maarufu wa soka hapa nchini.

 

Miongoni mwa mastaa waliohudhuria ni pamoja na Madee, Sholo Mwamba, Beki wa Yanga, Hassan Kessy, Man Fongo na wengine.

Mashabiki wa Stim Tosha wakifanya yao uwanjani.

Mpaka mwisho wa mchezo huo timu zote zilitoka suluhu ya bila kufungana hivyo kugawana pointi moja kila timu.

Shabiki wa stim Tosha akitamba uwanjani.

 

 

Mashabiki wakifuatilia burudani hiyo.

 

Wachezaji wa Stim Tosha wakiingia uwanjani kipindi cha pili cha mchezo huo.

 

Beki wa Yanga, Hassan Kessy akicheka kufuatia burudani zilizokuwa zikiendelea uwanjani hapo.

 

Shabiki wa StimTosha akiweka mambo sawa dakika za lala salama.

 

 

 

Hekaheka uwanjani zikishika nafasi.

 

 

Mchezo ukiendelea.

Ambulance likiwa tayari kwa dharula yeyote uwanjani hapo

PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply