The House of Favourite Newspapers

Uganda Yazindua Gari la Kivita Lililoundwa Nchini Humo

0

KAMANDA wa vikosi vya ardhi nchini Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameweka kwenye Twitter picha ya kile anachosema kuwa gari la kwanza la kivita kutengenezwa nchini humo.

 

Anasema “Liliundwa na kutengenezwa ncini Uganda”, lakini hakutoa maelezo kuhusu muundo na gharama yake. Gari hilo lililopewa jina la Chui – lilizinduliwa na baba yake, Rais Yoweri Museveni.

 

Jeshi la Uganda mwaka jana lilihusika katika msako mkali dhidi ya maandamano yaliyotikisa mji mkuu, Kampala, kufuatia kukamatwa kwa mgombea urais Bobi Wine. Maafisa walitetea utumizi wa silaha za moto, wakisema polisi na jeshi walikua wakikabiliana na waandamanaji.

Leave A Reply