Yanga Yaiwekea Mtego Azam FC

OFISA Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa, amefunguka mipango yao ya kuwamaliza Azam kwenye mchezo
wa ligi kuu.


Yanga itacheza na Azam FC,
Oktoba 30, mwaka huu katika Dimba la Benjamin Mkapa, huku ikiwa na historia ya kufungwa bao 1-0 za Azam kwenye mchezo wao wa mwisho.


Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii
jana walikuwa Songea wakicheza na KMC ukiwa ni mchezo wao wa raundi ya tatu ya ligi kuu na Azam walikuwa wakiumana na Namungo pale Chamazi, Dar.


Akizungumza na Championi
Jumatano, Senzo alisema kwamba, baada ya mchezo wao na KMC, kuisha kikosi  kitarejea moja kwa moja kambini tayari kwa maandalizi dhidi ya Azam FC.


“Tukimaliza mchezo salama,
mapema kesho (leo) tutarejea Dar es Salaam, kwa ajili ya maandalizi yetu na Azam FC, maana tunaona tutakuwa mchezo mzuri na wenye ushindani ila tumejipanga kushinda mchezo huo bila kuruhusudroo wala kufungwa.

 

“Tuna imani na mwalimu na benchi lake la ufundi watafanya vizuri ili kutusaidia kuweza kupata matokeo ya uhakika katika mchezo huo muhimu, kwani tumepania kuifuta kabisa historia yakufungwa na Azam FC, japo mpira huwa hautabiriki, ili hatutaruhusi kufungwa,” alisema Senzo.

Stori: Musa Mateja na Careen, Oscar, Dar es Salaam


Toa comment