The House of Favourite Newspapers

Uholanzi kuweka masharti mapya katika upelekaji wa teknolojia, China kutokana na sababu za kiusalama

0
Waziri Mkuu wa Uholanzi, Mark Rutte, akiwa na Rais Joe Biden.

Serikali ya Uholanzi imesema kwamba inapanga kuweka masharti mapya kwa upelekaji wa teknolojia za computer nchini China, ili kulinda usalama wake wa taifa.

Uholanzi inaonekana kujiunga na Marekani ambayo ilitangaza hatua sawa na hiyo hapo awali. Oktoba mwaka jana Marekani iliweka kanuni mpya kwenye upelekaji wa vifaa vya kutengeneza chip za computer nchini China, lakini kwa hilo kufaulu, inahitaji ushirikiano wa mataifa kama Uholanzi na Japan ambayo pia hutengeneza vifaa hivyo.

Mataifa hayo washirika yamekuwa kwenye mazungumzo kushusu suala hilo kwa miezi kadhaa. Waziri wa biashara wa Uholazi Liesje Schreinemacher ametangaza uamuzi huo kupitia barua kwa bunge, akisema kwamba hatua hiyo itaanza kutekelezwa kabla ya msimu wa joto kuanza.

Barua yake haikutaja China moja kwa moja ambayo ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa Uholanzi, wala kampuni ya ASML Holding NV, ambayo ni kubwa zaidi ya teknolojia barani Ulaya, na mshirika wa karibu wa mataifa yanayotengeneza vifaa vya semiconductor.

RAIS SAMIA AMTANIA MBOWE na LEMA – ”UMEKULA ASALI, TWENDE HIVYO HIVYO”…

Leave A Reply