The House of Favourite Newspapers

UIGIZAJI WAMKOSESHA DUMA MKE

0
Daud Michael ‘Duma’.

MWIGIZAJI wa kiume wa sinema za Kibongo, Daud Michael ‘Duma’ ameeleza namna alivyokosa mke, kisa kazi ya uigizaji na kuishia kuzaa na mwanamke huyo kabla ya kufunga ndoa.

Duma aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, sababu ya kuchelewa kuoa ni kisa hicho ambapo alipata mchumba na kufanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja lakini alipokwenda kwa wazazi wake na kujitambulisha kuwa anataka kumuoa binti yao walikataa kwa kuwa yeye ni msanii wa sinema za Kibongo.

“Kiukweli sisi wasanii tunaogopwa sana hasa kwenye suala la mapenzi, yaani nimeshidwa kuoa kwa sababu mimi ni msanii, kwa sasa nipo tu hata sijui nitaoa lini,” alisema Duma.

STORI: GLADNESS MALLYA| IJUMAA WIKIENDA

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

 

Leave A Reply