Ukaribu wa Lulu Diva Mama D Wazua Maswali

BAADA ya msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ na mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassimu ‘Sandra’ kuonekana wakiwa karibu, wamejikuta wakizua gumzo la aina yake.

 

Wawili hao walionekana wakiwa pamoja kwenye tamasha la Super Women lililofanyika Machi 8, mwaka huu ambayo ni Siku ya Wanawake Duniani ambapo Kampuni ya Wasafi inayomilikiwa na Diamond, ilitoa tuzo kwa wanawake bora.

 

Kutokana na ukaribu huo, wafuasi wengi wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram, walipoiona picha waliyopigwa wakati wa ishu hiyo wakiwa karibu, walizua gumzo na kujiuliza ukaribu wao unatoka wapi au unatokana na nini.

 

“Huu ukaribu wa mama D na Lulu Diva umeanza lini? Ngoja tusubiri mwisho wake maana yanaanzaga hivihivi,” ilisomeka moja ya komenti za mashabiki Instagram.

Toa comment