The House of Favourite Newspapers

Ukweli Shusho Kunaswa na Pombe

0

WIKIENDI iliyopita kumeibuka mjadala mkali kufuatia mwimba Injili na mchungaji maarufu Bongo, Christina Shusho kunaswa akinywa kitu kilichodaiwa ni aina ya bia ambapo yalisemwa mengi, hasa kwenye makundi ya WhatsApp ya watumishi wa Mungu.

 

Baadhi ya watu walikwenda moja kwa moja na kutoa hukumu kuwa, ndivyo walivyo watumishi wengi wa Mungu ambao wanajivika ngozi ya kondoo mbele za watu, lakini nyuma ya pazia ni watenda maovu.

 

Video hiyo ya shusho ambayo gazeti hili lina nakala yake, ni kweli inamuonesha akiwa ukumbini akinywa kinywaji hicho kilichopo kwenye chumba inayofanana naya bia ya kijani, lakini eneo la jina la kinywaji hicho limefichwa na tishu aliyotumia kushikilia kwani inaonekana kinywaji hicho kilikuwa ni cha baridiii.

 

Hata hivyo, baada ya mambo kuwa mengi, Shusho amejitokeza na kuanika ukweli wa jambo hilo akisema hiyo siyo pombe, lakini akawashukuru watu kwa kumjali na kumtaka kuwa kwenye mstari.

 

Shusho; kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameandika; “Tamko rasmi. Kwanza nawapenda bure. Pili nawashukuru kwa kujali maisha yangu ya kiroho. Tatu hapo ni kanisani Congo linajulikana kama Foundation Olangi Wosho. Nne kesho (jana) tusikose ibada.”

 

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba kuna aina ya juisi ya zabibu nchini Kongo ambapo imewekwa kwenye chupa ambayo inafanana na bia.

STORI; IJUMAA WIKIENDA, DAR

Leave A Reply