The House of Favourite Newspapers

Ulevi noma

0

konda1Konda huyo akiwa amelewa chakali.

Mashaka Kisusi, Mwanza
CHAPOMBE! Kondakta wa daladala moja la Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza amejikuta akiponzwa na ulevi baada ya bosi wake kuamua kumfukuza kazi mara moja, kufuatia kulewa akiwa kazini na kushindwa kufanya kazi, Risasi Jumamosi linaripoti.

Konda2Tukio hilo lilitokea mchana wa Jumatano iliyopita katika mnada wa Masasi wilayani Misungwi mkoani hapa, wakati kondakta huyo alipokuwa katika foleni ya kupakia abiria na kuamua kunywa pombe ya viroba iliyomzidia hadi kujikuta akipiga usingizi uliomfanya ashindwe kuwajibika kazini, hadi alipokutwa na bosi wake aliyefahamika kwa jina moja la Peter, ambaye pia ndiye dereva wa gari hilo.

Konda3“Baada ya zamu yake kufika, alikuwa hoi kabisa na kujikuta akishindwa kufanya kazi maana hata kusimama ulikuwa ni mtihani. Kuona hivyo, bosi wake ambaye ndiye dereva wa gari hilo alichukia sana ndipo alipoamua kuchukua maamuzi magumu ya kumuachisha kazi papo hapo,” alisema shuhuda wetu.

Mpaka shuhuda wetu anatoka eneo la tukio kondakta huyo alikuwa bado yuko chakari.

Leave A Reply