The House of Favourite Newspapers

Ulinzi Waimarishwa Katika jiji la Arusha Kuelekea Uzinduzi Wa Royal Tour AICC Kesho

0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amewaambia wananchi Kuwa hali ya ulinzi na usalama katika jiji laArusha na Mkoa ni shwari kuelekea uzinduzi wa filam ya The Royal Tour.

 

Kamanda Masejo amesema kuwa Kuelekea uzinduzi wa filamu maalum ya TheRoyal Tour Tanzania Kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo limejianga vyemakuhakikisha dunia inashuhudia uzinguzi huo wa filamu ya the Royal Tour itakayo fanyika siku ya kesho 28.04.2022 katika kituo Cha kimataifa Cha Mikutano Arusha AICC.

 

Kamanda Masejo amesema kama ilivyo desturi ya wakazi wa jiji la Arusha kuwa wakarimu kwa wageni basi vyema wakaionyesha dunia ukarimu huo na kuionyesha dunia kuwa Arusha ni kitovu Cha utalii.

Leave A Reply