The House of Favourite Newspapers

Usiku wa wakongwe…Bongo Fleva kutawala mkesha Pasaka

0

USIKU wa wakongwe wote wa Muziki wa Bongo Fleva unatarajiwa kufunika Mkesha wa Pasaka (Machi 26) ndani ya Fukwe za Sunrise-Kigamboni jijini Dar.

Akizungumza na Showbiz, mratibu wa shoo hiyo, Majid Mdoe ‘Promota Bonga’ alisema kuwa siku hiyo itakuwa maalum kwake kwa kuwa atakuwa akitimiza miaka 25 tangu kuwa promota wa wasanii Bongo.

“Pazia la burudani linatarajiwa kufunguliwa kuanzia saa nne asubuhi ambapo kutakuwa na michezo mbalimbali kama vile mpira wa mchangani, jogging, fasheni shoo na mingine mingi na usiku ambao ni mkesha kutakuwa na wakongwe wote wa Bongo Fleva ambao ni Jaffarai, Afande Sele, Nature, Dully, Abby Skillz, Gangwe Mobb na wengine wengi,” alisema Bonga na kumalizia kuwa kiingilio getini kitakuwa sh. 10,000 tu.

Leave A Reply