The House of Favourite Newspapers

Usiku wa ya Kale ni Dhahabu.. Dar Live patakuwa hapatoshi

0

hadijayusufHadija Yusuf.

Stori: Mwandishi Wetu, RISASI JUMAMOSI

UWANJA wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar, unatarajiwa ‘kubanana’ pale vikundi vya Muziki wa Taarab zaidi ya ishirini vikiongozwa na Mzee Yusuf, Patricia Hilary na Khadija Kopa vitakapopanda jukwaani Mei 21, mwaka huu na kuporomosha shoo ya kihistoria.

khadija_kopa1Khadija Kopa

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo aliwataja wakali watakaoweka historia kuwa ni Leila Rashid, Hadija Yusuf, Bi Mwanahawa, Joha Kassim kutoka Jahazi Modern, Hadija Kopa, Otham Sudi, Mwanaidi Shaban kutoka Muungano, Shakira kutoka J.K.T, Misambano na Kisauji kutoka Babloom na wengine kibao.

“Utakuwa ni usiku wa kukumbukwa na kila mmoja kwa maana kuwa itakuwa ni mara ya kwanza kwa vikundi hivyo kukutana katika jukwaa la Dar Live,” alisema Mbizo.

Wakali wengine wanaotarajiwa kuwepo ni Sabaha Mchacho, Sihaba Juma, Hassan Soud, Thabit Abdul, Bi Afua, Sizya Mazongela, Mustafa, Sihaba Juma, Zubeda Mlamali na wengine.

Shoo hiyo inadhaminiwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel kupitia huduma ya Airtel Money Taptap.

Leave A Reply