The House of Favourite Newspapers

Utata Mtupu Kuvunjika Ndoa ya Will Smith

0

UTATA mkubwa umeibuka juu ya kuvunjika kwa ndoa ya staa mkubwa duniani, mwanamuziki na mchekeshaji wa Marekani, Will Smith na mkewe Jada Pinkett.

 

Wikiendi iliyopita kuliibuka mjadala wa dunia, baada ya mwanamuziki dogo wa Marekani, August Alsina kuweka wazi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi wa muda mrefu na Jada.

 

August alifanya mahojiano exclusive na Televisheni ya Power On Five ambapo alithibitisha hilo.

“Nimekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Jada kwa miaka mingi, kiukweli nilimpenda na ninampenda mno.

 

“Nilijikabidhi kwake kwa kila kitu, kiasi kwamba naweza nikafa sasa, nikijua kuwa nilijitoa kiukweli na baadhi ya watu hawapati mapenzi haya katika maisha yao,’’ alisema August.

 

Dogo huyo aliongeza kuwa alipewa ruhusa na Will Smith, kwani wawili hao wapo kwenye ndoa ya wazi (open marriage) ambayo ni ruhusa kuwa na uhusiano mwingine nje, japo wamekuwa wakikanusha hilo.

 

Baada ya intavyu ya dogo huyo, Will Smith alijitokeza na kukanusha vikali juu ya madai ya kumruhusu jamaa huyo kuchepuka na mkewe Jada ambaye wamedumu kwenye ndoa kwa miaka 23.

Katika kipindi chote cha ndoa yao wamejaaliwa watoto wawili, Willow Smith na Jaden Smith.

STORI: HAPPYNESS MASUNGA

Leave A Reply