The House of Favourite Newspapers

Uviko-19 Yasababisha Wafanyakazi Nchini Australia Kufanyia Kazi Nyumbani Kwao

0
Raia nchini Australia wameaswa kufanyia kazi nyumbani kuepuka ongezeko la maambukizi mapya ya Uviko-19

WAFANYAKAZI nchini Australia washauriwa kufanyia kazi nyumbani kutokana na ongezeko kubwa la maambukizi ya virusi vya Uviko-19 kulikumba Taifa hilo.

 

Mamlaka zimebainisha kuwa jumla ya kesi 300,000 za maambukizi mapya ya Uviko 19 zimeripotiwa kwa kipindi cha siku saba zilizopita.

 

Nchi ipo katika awamu ya tatu ya wimbi la maambukizi ya virusi vya Uviko 19 ambapo kwa siku moja imeripotiwa maambukizi mapya yamefikia 50,248 ikiwa ni kiwango kikubwa kurekodiwa kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita.

 

Jumla ya raia 5,239 wa Australia wapo hospitali wakiendelea kupatiwa matibabu kwa maambukizi ya Uviko-19.

Raia wamekuwa wakipimwa mara kwa mara juu ya maambukizi ya Uviko-19

“Tunatakiwa kufanya baadhi ya mambo kwa namna nyingine angalau kwa kipindi kifupi.” Alisema Mkuu wa tiba wa nchi ya Australia.

 

Aliendelea kwa kusema:

 

“Tunatambua kuwa kufanya kazi tukiwa nyumbani ni njia muhimu ya kusaidia kutatua changamoto hii tunayoiita maambukizi ya haraka ya Uviko-19.”

Kumekuwa na ongezeko kubwa la maambukizi mapya ya wagonjwa wa Uviko-19kwakipindi cha siku saba zilizopita

Aidha Waziri Mkuu wan chi hiyo Anthony Albanese ametoa rai kwa waajiri kuangalia namna ya kukubaliana na wafanyakazi wao ili kurahisisha mkakati huo wa Serikali kuweza kufanya kazi kwa ufanisi.

Leave A Reply