The House of Favourite Newspapers

Uwoya afyatuka kuitwa jini

0

IRENE Pancras Uwoya au Mama Krish ni mwigizaji mkubwa wa Bongo Movies ambaye amefyatuka kwa ukali akisema kuwa, hakuna kitu asichokipenda kama jina jipya alilopewa na baadhi ya watu mitandaoni la Jini.

 

Uwoya anasema kuwa, hii ni kwa sababu jina hilo linaweza kukua na kumtengenezea vitu tofauti kabisa katika maisha yake kwa sababu siku zote maneno yanaumba.

 

Uwoya ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, kuitwa jina hilo kuna uwezekano mkubwa hata hao majini wenyewe wanaweza kumfuata na kumsababishia matatizo mengine makubwa maishani mwake.

 

“Yaani kiukweli kabisa hakuna jina ambalo ninalichukia kama kuitwa Jini. Kwanza linaweza kuathiri kabisa maisha yangu ya kila siku,” anasema Uwoya anayesemekana ana pesa zake mjini.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply