The House of Favourite Newspapers

Uwoya Atoa Ahadi ya Kugharamia Kila Kitu Harusi ya kajala na Harmonize

0
Uwoya amesema atagharamia harusi yote ya Kajala na Harmonize

Muigiza wa Maarufu wa Filamu za Bongo Supastaa Irene Uwoya ametoa ahadi ya kugharamia kila kitu kwenye harusi ya Kajala na Harmonize kama wawili hao wataamua kufanya hivyo.

 

Uwoya anayefahamika kama msanii na supastaa anayekuja bata na hachungulii pesa amethibitisha hilo katika duka lake la Lizypayless Wedding Mall ambalo linajihusisha na shughuli za kuhudumia vifaa na mahitaji mbalimbali ya harusi.

Irene Uwoya Muigizaji

Kuhusu uhusiano wa Kajala na Harmonize, Uwoya amesema yeye hana tabia ya kuingilia mahusiano ya watu kama ambavyo yeye hapendi kuingiliwa katika uhusiano wake hivyo kama Kajala ana furaha kuwa na Harmonize basi yeye pia atamsapoti kwani hicho ndicho kitu muhimu katika maisha.

Harmonize na Kajala

Kwa upande mwingine Uwoya ametoa ofa ya kumgharamia mtu yeyote yule ambaye anatamani kuolewa lakini hana uwezo wa kugharamia gharama za harusi na haijalishi kama ni staa au siyo staa.

 

 

 

 

 

 

Leave A Reply