The House of Favourite Newspapers

Uwoya Avimba na Range Rover ya Bei Mbaya

0

God is good all the time (Mungu ni mwema muda wote! Hayo ni maneno ya staa wa Bongo Movies, Irene Uwoya alipokuwa akilitambulisha kwa mara ya kwanza ndinga lake aina ya Range Rover Sport HSE.

 

 

Kwa sasa ukikutana na Uwoya au Mama Krish akiwa anavimba mjini na Range Rover lenye rangi nyeusi, usifikiri ameazima, ni la kwake.

 

Kwa mujibu wa Uwoya, gari hilo linatokana na jasho lake kwenye uigizaji ambao ameufanya kwa zaidi ya miaka kumi akiongezea na biashara zake nyingine.

 

 

Uwoya amekuwa akiposti picha mbalimbali akiwa na gari hilo la bei mbaya kiasi cha kuwatoa udenda mabinti wa mjini wanaopenda maisha mazuri.

 

“Nilikopitia ungepita wewe ungeweza kufa,” aliandika Uwoya kwenye ukurasa wake akisindikiza na picha akiwa na gari hilo.

Kwenye picha nyingine amesimama na kuliegemea gari hilo kwa mbele na kuandika; “God is everything (Mungu ni kila kitu).”

 

Uwoya anasema kwa upande wake hayo ni matunda ya kujituma kwake na kwamba kila mtu akijituma atafikia malengo yake.

Si mara ya kwanza kwa Uwoya kumiliki gari kama hilo kwani miaka mitano iliyopita alikuwa na gari la aina hiyo.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, fundi ambaye ni mtaalam wa kupandisha magari hadhi aitwaye Raider anasema kuwa, kwa sasa gari kama hilo la Uwoya si chini ya shilingi milioni 200 kama mtu anataka kulimiliki.

Leave A Reply