The House of Favourite Newspapers

Wazee wa Kusafirisha Vinyonga Watiwa Mmbaroni, Kesi ya Uhujumu Uchumi

0

WAFANYABIASHARA watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kujihusisha na biashara wa nyara za Serikali kwa kusafirisha na kupokea vinyonga 74 wa Shilingi Milioni 8.5  bila kuwa na kibali.

Washtakiwa hao waliofikishwa mahakamani hapo ni, Erick Ayo, Ally Ringo na Azizi Ndago. Wamesomewa mashtaka yao na wakili wa Serikali Kija Luzungana mbele ya hakimu mkazi mkuu, Huruma Shaidi.

kabla ya kusomewa mashtaka yao hawakutakiwa Hakimu alisema washtakiwa hawatatakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama ya Kisutu kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi kibali maalum kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP).

Wakili Luzungana amedai washtakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya Februari 22, 2020 na Februari 22, 2021 katika maeneo tofauti ya Mkoa wa Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Pwani.

Katika shtaka la pili, siku na maeneo hayo washtakiwa hao waliongoza genge la uhalifu kwa kujihusisha na biashara ya nyara za Serikali bila kuwa na kibali kwa kukusanya, kusafirisha na kupokea vinyonga 74  bila kuwa na kibali.

Upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na ukaomba  tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 29 mwaka huu licha ya hakimu kueleza kuwa kwa kuwa kiwango cha fedha kipo chini ya Mil 10 washtakiwa wanaweza kupata dhamana lakini wameshindwa kutimiza masharti.

Leave A Reply