The House of Favourite Newspapers

Uwoya: He! Mimi Mjamzito?

0

Stori: Brighton Masalu | IJUMAA WIKIENDA

DAR ES SALAAM: Sexy lady wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krish’ amefungukia madai kuwa, kwa sasa ametengeneza urafiki wa muda na ndimu, samaki wabichi na ukwaju kwa kinachosemekana ni mjamzito.

Huku akionesha kushtushwa na habari hizo zinazoenezwa bila kutaja mhusika wa kibendi hicho, Uwoya alikuwa na haya ya kusema:

“He! Mimi? Mjamzito? Jamani imekuwa too much (imezidi), watu wanaongea kama hawana mambo ya kufanya maishani, kinachowashtua wengi ni mabadiliko ya mwili wangu. Unajua nimenenepa kwa kweli, inafika mahali mtu anaridhika na maisha.

Mwili nao unabadilika kutokana na sababu za kibaiolojia, sina njaa kama zamani. Napata madili mengi, hivyo lazima niridhike na kunenepa, wengi wanadhani ni mimba na hata familia yangu, walidhani ni hivyo, lakini sina mimba na hata sifikirii kufanya hivyo kwa sasa,” alisema Uwoya.

ILIKUPITA HII? Uwoya, Kibonge Sexy na Vita Ya Mapenzi

Leave A Reply